Spinach yenye maziwa na nazi

Mboga za majani ni rahisi kupatikana, kuandaa na pia chanzo kizuri cha virutubisho muhimu mwilini. Mapishi haya ya spinach yanatumia maziwa na nazi ili kuipa ladha tamu, harufu nzuri na mvuto kwa mlaji. Unaweza kuongeza viungho vingine unavyopenda ili kuipa ladha mboga yako.

Mahitaji

 • Spinach
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Maziwa vijiko 100mls
 • Tui zito la nazi, 100mls
 • Kitunguu
 • Pilipili hoho
 • Mafuta ya kula, vijiko 2 vikubwa
 • Kitunguu saumu kijiko 1 kidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kula spinach hii kwa ugali, wali au chakula kingine unachopendelea. Uwepo wa viungo vingine hukupa ladha tamu zaidi kwenye hii spinach.

 • Andaa kitunguu, pilipili hoho. Kata vipande vidogo hifadhi pembeni.
 • Andaa spinach, osha kisha hifadhi vizuri pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni kwenye moto mkali. Acha sufuria ipate moto, weka mafuta ya kula. Weka spinach. Koroga vizuri kisha funika na mfuniko. Acha kwa dakika 1 kisha koroga halafu toa hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni, acha ipate moto vizuri. Unaweza kutumia sufuria uliyotumia kupikia spinach. Weka mafuta, weka kitunguu maji, koroga vizuri. Weka kitunguu saumu na pilipili manga na chumvi. Koroga vizuri. Weka pilipili hoho, koroga vizuri. Acha kwa dakika 2 vichemke pamoja.
 • Weka spinach, koroga vizuri. Hakikisha moto ni mkali. Weka tui la nazi, koroga hadi tui lianze kuchemka. Weka maziwa, koroga vizuri. Acha ichemke kwa dakika 3 kisha epua.
 • Mboga yako iko tayari kuliwa.

misosi-spinach-maziwa-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Cutlets za pilipili
dakika 5
Walaji: 4

Wali wenye nazi na maziwa
dakika 20
Walaji: 2

Nyama tamu yenye pilipili
dakika 25
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.