Spring shrimp rolls

Spring shrimp rolls, mie nazipenda. Unaweza kuziandaa kisha ukahifadhi kwenye jokofu na kuzikaanga kwa muda mchache pale unapohitaji. Binafsi huzitengeneza kwa wingi na kuhifadhi kwenye jokofu ili nile wakati nnapokuwa na hamu ya chakula chepesi na cha haraka. Unaweza pia kufanya hivyo, maana kwa sasa una jinsi ya kuandaa hiki chakula. Kazi kwako.

Mahitaji

 • Springroll wrappers au rice wrappers, uweza kuzipata supermarkets au maduka yanayouza bidhaa za vyakula asili ya Asia – India na china.
 • Uduvi (Shrimp) au kamba (prawns)
 • Tangawizi 1, menya kisha saga
 • Karoti 2, kata kisha saga
 • Kitunguu saumu 1, menya kisha ponda
 • Kitunguu maji, kata kitunguu vipande vidogo
 • Soy sauce vijiko 2 vikubwa
 • Mafuta ya kula
 • Unga wa ngano vijiko 2 vikubwa
 • Maji ¼ kikombe
 • Chumvi ½ kijiko kidogo
 • Kabichi, kata vipande vyembamba sana.

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Spring rolls ni kitafunwa kizuri cha hamu ambacho unaweza kula kama kitafunwa, kiambato cha chakula kikuu au kama kichangamsha mdomo wakati wa maongezi. Ni chaguo lako.

misosi-rolls-main2

 • Andaa kila kitu kisha changanya vizuri – kitunguu maji, kitunguu saumu, tangawizi na kabichi. Koroga vizuri mchanganyiko hadi uchanganyike vizuri. Weka chumvi. Endelea kukoroga vizuri.
 • Andaa uduvi au kamba – kata mikia, toa magamba magumu. Kama wakubwa sana unaweza kukata katikati au kwenye vipande vidogo unavyopenda. Mie nimewatumia wakiwa wazima bila kuwakata vipande.  Changanya uduvi kwenye bakuli yenye mchanganyiko wa mboga za majani. Koroga vizuri. Hakikisha vinachanganyika vizuri kabisa.
 • Kwenye bakuli ndogo tofauti, changanya unga wa ngano na maji. Koroga vizuri hadi uwe uji wenye uzito wa wastani. Weka pembeni. Hii utatumia katika kufunga rolls zako ukishajazia mboga na uduvi.
 • Toa wrappers kwenye mfuko, weka juu ya chombo kisafi au sehemu safi yenye nafasi unayoweza kuweka chakula.

Hakikisha wrappers zisiwe ngumu maana hazitoweza kukunjika vizuri, na matokeo yake itakatika. Kama wrap ni ngumu unaweza kuzihifadhi katikati ya vitambaa vyenye unyevunyevu ili ziwe laini.

 • Tandaza wrappers vizuri, weka mchanganyiko wa mboga za majani na uduvi juu yake. Hakikisha vimeenea vizuri. Anza kukunja vizuri ili mboga mboga zote ziwe kwa ndani. Mie nimeacha uduvi ametokeza ili kuleta mvuto, lakini unaweza kumziba ili apate kuiva vizuri akiwa kwenye mafuta. Kabla hujamalizia kuzungusha wrappers, paka uji wa  ngano kwenye kipande kidogo kilichobakia ili wrapper ipate kufunga vizuri na isifunguke. Hifadhi roll pembeni na rudia hii hatua kwa rolls nyingine hadi umalize.

misosi-spring-rolls-main3

 • Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto vizuri. Weka mafuta ya kula, yawe mengi kiasi ili rolls ziive vizuri. Acha yapate moto, kama nyuzijoto 180°C, kisha weka rolls. Kutegemea na chombo, weka roll lakini angalie zisipandiane. Acha ziive vizuri, takribani dakika 7 hadi 8. Zikianza kubadilika rangi epua kisha hifadhi pembeni ili zichuje maji. Rudia hii hatua kwa rolls zilobaki hadi umalize.
 • Tenga vizuri na upate raha ya rolls.

misosi-spring-rolls-main0


MAPISHI YAPENDWAYO

Chips na nyama ya ng'ombe
dakika 25
Walaji: 2

Nyama tamu ya ng'ombe
dakika 40
Walaji: 4

Sambusa za mboga za majani
dakika 20
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.