Supu ya kuku

Supu ya kuku yenye ladha tofauti kutokana na mchanganyiko wa mboga za majani. Inaweza kuliwa na mkate, maandazi, ikiwa tupu au vingine upendavyo.

Mahitaji

 • Kitunguu
 • Pilipili hiho
 • Viazi 5
 • Kuku nusu
 • Carrot
 • Limao/ndimu
 • Tangawizi
 • Pilipili manga
 • Tambi za mchele (kidogo sana)
 • Unga wa ngano kiasi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Kata vipande vya kuku na kuviosha.
 • Kamulia limao kwenye nyama. Weka chumvi, tangawizi na kuacha mchangayiko kwa dakika 10 ili viungo vipate kuingia kwenye nyama.
 • Andaa pilipili hoho, kitunguu, karoti kwa kukata vipande vidogo vidogo unavyopenda.
 • Menya viazi, osha na kisha kata kwenye vipande vidogo ili viweze kuiva kirahisi.
 • Bandika nyama jikoni. Usiongeze maji. Acha machi yaliyomo  yajichuje, ichemke hadi maji yakauke.
 • Maji ya nyama yakikauka, ongeza maji kiasi - kikombe 1 kikubwa na kuiacha ichemke.
 • Ikianza kuchemka - weka pilipili hoho, kitunguu, viazi, tambi, pilipili manga na karoti kwenye nyama.
 • Koroga unga wa ngano kwenye bakuli la maji ya uvuguvugu hadi mchanganyiko uwe laini. Kisha changanya kwenye supu.
 • Acha mchanganyiko uchemke hadi viazi viive.
 • Ukiwa mpenzi wa pilipili weka pilipili ikiwa mbichi ili kuipa supu harufu nzuri ya pilipili.
 • Toa jikoni na tenga mezani. Supu yako iko tayari kurambwa.
 • Usisahau kunyunyuzia limao wakati wa kuinywa, maana uchachu wa limao huongeza ladha zaidi kwenye ulimi wako.

Jirambe….


MAPISHI YAPENDWAYO

Chocolate Fondant Pudding
dakika 20
Walaji: 8

Koni za asali
dakika 25
Walaji: 10

Toa maoni yakoDavid
12:15, Sat 01 Nov 2014
Elimu nzuri saana ya chukula kilicho bora inapatikana humu, Nafikiri hii ni site bora ya kiswahili hapa Tanzania, inafaa watu wengi waitambue na waitembelee waweze kujifunza. Binafsi nimejifunza vingi saana. Hongera na endelea kufundisha jamii.
Charlotte Misosi
13:33, Mon 03 Nov 2014
@David, karibu sana kwenye tovuti yetu ya Misosi.
Asante sana na tunashukuru kwa maelezo yako. Sisi tunajitahidi pia kuweka vitu vinavyoelimisha zaidi jamii. Hakuna kilicho kizuri kama kufahamu kuwa unafurahia yale tunayoandika na kuelimisha watu kwa moyo mmoja.

Karibu sana na endelea kufaidika na ujuzi tunaoutoa, asante kwa kuchangia. Tumefurahi sana.
Endelea kufaidika na mambo mengi zaidi juu ya misosi na afya.
JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.