Supu ya Kuku

Supu ni kitu pekee ninachopenda kutumia wakati nataka kujiiwaza na kuwa na muda mzuri peke yangu. Ni kitu muhimu kunywa nikiwa najisikia uchovu, maumivu ya kichwa au kikohozi. Uwepo wa limao kwenye hii supu hufanya koo langu kusuuzika na kufurahi. Ni rahisi kuandaa lakini ina utamu wa kipekee na harufu ya kukufanya uwe na hamu ya kula.

Mahitaji

 • Kuku vipande 4 (Unaweza kuwa na vipande vya kuku wa kienyeji au wa kisasa)
 • Karoti 2
 • Pilipili mbuzi (au yeyote unayopenda)
 • Chumvi
 • Kitunguu kikubwa 1
 • Tangawizi 1 iliyopondwa
 • Limao 1
 • Pilipili hoho 2 (Huwa natumia pilipili hoho zenye rangi tofauti kupata rangi nzuri ya chakula)
 • Unaweza pia kuongeza majani na viungo unavyopenda

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa kuku, kata vipande tofauti.  Osha, usitoe ngozi. Weka kwenye sufuria kubwa inayotosha. Kamulia limao, weka chumvi. Weka tangawizi. Koroga vizuri. Bandika jikoni, funika na mfuniko. Acha nyama ichemke ichuje maji yake kwa muda.  Maji yakianza kupungua, ongeza maji mengine kisha acha ichemke kwa dakika 5.
 • Andaa pilipili hoho, kitunguu, na karoti – menya kisha kata vipande vidogo. Weka kwenye supu inayochemka. Koroga kiasi. Weka na pilipili ili ichemke na kutoa harufu nzuri kwenye supu. Usipasue pilipili maana itakuwa kali, acha itoe harufu nzuri tu.
 • Baada ya nyama kuiva, toa supu na tenga ujirambe.
 • Supu hii inaweza pia kuwekewa macaroni, tambi au mboga mboga tofauti za majani ili kuiongezea ladha.
 • Mie nimekula supu hii na mkate.

supu-kuku-misosi


MAPISHI YAPENDWAYO

sweet and sour chicken
dakika 25
Walaji: 2

Caramel cheese cake
dakika 60
Walaji: 5

Mkate wa zucchini na korosho
dakika 55
Walaji: 5

Keki ya nanasi
dakika 40
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.