Supu ya samaki yenye vionjo tofauti

Supu, chakula rahisi na kizuri kuandaa nyumbani kwa mlo wa bora na wa haraka. Supu ya samaki ni nzuri kuliwa muda wowote, maana ni chakula kilichojaa virutubisho na bora zaidi. Samaki ni watamu, ila angalia miba isikukwame tu. Maana unaweza kula ukadhani ni nyama.

Mahitaji

 • Samaki
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saumu, punje 3, menya kisha saga.
 • Karoti 1
 • Pilipili hoho 1
 • Kabichi ½
 • Mbegu za Koriandaa kijiko 1 kidogo
 • Viazi mbatata (mviringo) ¼ kilo, au unaweza kutumia ndizi mbichi
 • Kiungo cha mboga, mie nimetumia royco

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa samaki – toa magamba, toa utumbo na uchafu. Osha kisha weka samaki kwenye sufuria. Kama samaki mkubwa sana unaweza kumkata vipande vidogo ili atoshe kwenye sufuria na aive vizuri.
 • Menya kisha Kata kitunguu maji, karoti, na pilipili hoho. Weka kwenye sufuria yenye samaki. Kata kabichi kwenye vipande vya wastani, ongeza kwenye sufuria yenye samaki.
 • Menya viazi au ndizi kisha kata vipande vya wastani. Weka pia kwenye sufuria yenye samaki.
 • Weka kitunguu saumu na curry powder. Unaweza kuweka pilipili unazopenda ili kuleta ladha nzuri ya supu. Weka maji kidogo na chumvi kwenye sufuria. Bandika sufuria jikoni acha ichemke. Viazi vikianza kuiva, ongeza maji kiwango unachotaka cha supu.
 • Weka kiungo cha mboga, nimetumia royco, kama kijiko 1 kikubwa na mbegu za korianda. Funika na acha supu ichemke hadi uone ibaki kiwango unachotaka. Epua na tenga pembeni.
 • Unaweza kula supu hii kama yenyewe, kwa mkate, mihogo, maandazi, au chochote unachoamua. Tenga supu na ujirambe kwa raha zako.

misosi-supu-samaki-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Mchemsho wa samaki na ndizi
dakika 20
Walaji: 4

Pilau ya mboga mboga
dakika 35
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.