Supu ya ulimi wa ng'ombe

Supu ya ulimi ni mlo utakao kupa burudani na radha tamu sana, itakayokufanya ufurahie siku yako. Supu hii waweza kula na chapati au yenyewe. Na ukajiramba na utamu wake.

Mahitaji

 • Ulimi wa ng'ombe
 • Soy sauce
 • Ndimu
 • Kitunguu saumu
 • Chumvi
 • Pilipili mbuzi
 • Karoti
 • Maji

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Nunua ulimi ambao umeshatengenezwa kabisa.
 • Bandika sufuria jikoni, weka ulimi, weka chumvi, kamulia ndimu, weka vitunguu saumu na karoti.
 • Kata karoti vipande vidogo na vyembamba.
 • Weka maji ya kutosha .Funika Sufuria na mfuniko.
 • Ikikaribia kuiva weka soy sauce, hii inasaidia kuongeza ladha kwenye supu.
 • Onja kama nyama imeiva, kama tayari weka pilipili. Vilevile unaweza kuongeza pililipi ukishaipua supu toka jikoni.
  TIP: Kuongeza pilipili pembeni itasaidia  kuwafanya hata wale wasiotumia pilipili kunywa supu bila kupata adha ya ukali wa pilipili. Pia unaweza kuweka pilipili nzima (isiyokatwa au kupasuka) ili kuweka ladha tamu kwenye supu na kuacha ichemke kwa dakika chache kabla ya kuipua. Hii pilipili inaweza kuliwa na mtu anayeyependa kula pilipili. 
 • Hapo utakua tayari kujiramba na supu ya ulimi wa ng'ombe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kachori tamu zenye giligilani
dakika 20
Walaji: 6

Keki tamu ya mtindi na vanilla
dakika 50
Walaji: 8

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.