sweet and sour chicken

sweet and sour chicken ni rahisi kuandaa na haichukui muda mrefu,unaweza ukala wali au ukala yenyewe tu na ukafurahi. pia unaweza kutumia juice ya nanasi badala ya nanasi

Mahitaji

 • Kuku asiye ngozi wala mifupa nusu kilo
 • Cornstarch vijiko vitatu vya chakula
 • Mayai mawili tunatumia ute
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Vinegar kikome 1 cha kahawa
 • Sukari vijiko 3 vya chakula
 • Mafuta ya alizeti vijiko 5 vya chakula
 • Maji vijiko 5 vya chakula
 • Pilipili hoho 1kubwa
 • Kitungu maji 1 kikubwa
 • Karoti 1
 • Pilipili manga kijiko 1 cha chai
 • Nanasi au juice ya nanasi
 • Tangawizi kijiko 1 cha chai
 • Kitunguu saumu kijiko 1 cha chai
 • Soy sauce nusu kikombe cha kahawa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa kuku na muweke kwenye bakuli, chukua cornstarch weka kisha weka ute wa yai na chumvi changanya vizuri kisha weka kuku kwenye jokofu kwa dakika 45.
 • Menya nanasi katakata vipande vya mraba, pilipili hoho pia kata umbo la mraba na vitunguu maji. Menya karoti ikwangue upate vipande vidogo sana.
 • Weka pembeni viungo, mtoe kuku.
 • Chukua frying pan iwe non stick frying pan,weka jikoni ikipata moto weka vijiko 3 vya mafuta, yakipata moto weka kuku.
 • Kaanga mpaka awe wa kahawia mgeuze upande wa pili mkaange pia, mtoe kuku weka kwenye sahani safi.
 • Weka mafuta kwenye kikaangio au sufuria, yakipata moto weka kitunguu maji, pilipili hoho na vipande vya nanasi koroga kwa dakika 1.
 • Weka kitunguu saumu, tangawizi na karoti koroga bila kuacha kwa dakika 2.
 • Weka vinegar, sukari na ketchup koroga kwa dakika 3 weka soy sauce ikichemka weka kuku na acha achemke.
 • Chukua bakuli weka maji na vijiko 2 vya cornstarch koroga, weka huo mchanganyiko kwenye kuku huku ukiendelea kukoroga, usiache kukoroga tafadhari mpaka uone umeanza kua mzito kisha acha.
 • Acha achemke kwa dakika 3 kisha nyunyizia pilipili manga kisha epua na jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Bagia za kunde
dakika 7
Walaji: 4

Maandazi ya Vanila na Nazi
saa 1
Walaji: 15

Pound cake
dakika 60
Walaji: 4

Salad ya kabichi
dakika 5
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.