Sweet & Sour Chicken

Kwa wale wanaopenda vitamu, hii ni aina nyingine rahisi ya kuandaa sweet and sour chicken ya kuoka – nyama ya kuku yenye viungo vinavyoifanya iwe tamu na chachu wakati mmoja. Ni nyama nzuri inayoweza kuliwa na vyakula mbalimbali au kuliwa yenyewe kama kitafunwa kikisindikizwa na kinywaji laini. Huyu kuku amewekwa ketchup, sukari, juisi ya chungwa, red wine vinegar na sweet red chili pepper sauce.

Mahitaji

 • Vipande vya kuku – ½ 
 • Tomato Ketchup ½ kikombe
 • Red wine vinegar ½ kikombe (Au unaweza kutumia apple cider vinegar)
 • Sukari  ½ kikombe
 • Sweet red chili pepper sauce ¼ kikombe
 • Juisi ya chungwa 1/3 kikombe

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kama kuna viungo unavyopendelea kula na havimo unaweza kuongeza ili uongeze ladha ya huyu kuku.

 • Washa oven kwenye nyuzijoto 350°F (180°C) na acha ipate moto.
 • Safisha kuku – osha kwenye maji safi kisha kausha vizuri. Paka sinia au bakuli ya kuokea mafuta yasiyogana, au unaweza kuweka foil paper, kisha panga vipande vya kuku vizuri juu yake. Weka kuku kwenye oven na oka kwa dakika 35 hadi 40.
 • Kwenye bakuli kubwa, weka sukari, ketchup, red wine vinegar, juisi ya chungwa na pepper sauce. Koroga.
 • Bandika sufuria jikoni, weka mchanganyiko wa sauce ulioandaa. Kwenye moto wa wastani, koroga taratibu sauce hadi ianze kuchemka. Toa sauce kwenye moto kisha acha ikae kwa dakika 5.
 • Toa kuku kwenye oven, hakikisha wameiva vizuri.
 • Wakati kuku bado wa moto, chovya vipande vyote kwenye sauce uliyoandaa. Acha kuku wakae kwenye sauce kwa dakika 5 hadi 10. Koroga vizuri ili sauce ienee vizuri kwenye nyama ya kuku.
 • Unaweza kujiramba. Ni kuku anayeliwa kwa chakula chochote upendacho.

sweet-sour-misosi-chicken-poor


MAPISHI YAPENDWAYO

Salad yenye yai na samaki
dakika 0
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.