Tambi na mayai

Chakula kitamu, rahisi kuandaa na kinachoweza kuliwa wakati wowote ule. Jaribu mapishi haya na upate kujua ladha tamu ya maisha.

Mahitaji

 • Vitunguu 2
 • Mayai 2
 • Tambi
 • Mafuta ya kula
 • Chumvi
 • Kitunguu saumu cha unga

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaandaa chakula kitamu, chenye afya lakini pia kinavutia haswa. Tukimaliza kupika tutakuwa na sahani inayoonekana hivi.

20141218_203453

Unaweza kuandaa hivi vitu wakati mmoja, maana muda unatosha. Hapa chini naweka maelezo tofauti ili iwe rahisi kuelewa.

20141218_200523

Andaa Tambi

Kabla hujaanza kupika tambi angalia muda unaoshauriwa kuzipika kama ilivyo kwenye maelezo. Muhimu kufahamu muda ili kupata matokeo mazuri.

 • Bandika sufuria ya maji jikoni. Weka chumvi kiasi.
 • Weka tambi unazoweza kumaliza. Hakikisha usizikate katikati. Weka ziegemee upande wa sufuria, zikipata moto vizuri zitaingia zote kwenye sufuria.
 • Baada ya dakika 6 hadi 7 hakiki kama tambi zimeiva na kiini kimelainika.  

Hakikisha tambi zinakaa kwenye maji dakika moja pungufu ya muda ulioshauriwa kwenye maelezo yake. Hii huzifanya tambi ziive vizuri lakini zisiwe kama uji. Zikiiva sana huwa zinagandana na kuwa kama uji.

 • Tambi zikiiva, toa na weka pembeni kwenye sahani.

Andaa Mayai

 • Menya vitunguu. Kata vipande vidogo. Tenga pembeni.
 • Bandika kikaango (frying pan) jikoni. Weka mafuta, acha yapate moto kiasi.
 • Pasua yai. Weka chumvi, koroga vizuri.
 • Weka kitunguu saumu kwenye kikaango. Weka kitunguu kwenye kikaango. Koroga kiasi na acha viive kiasi.
 • Baada ya dakika 2 – 3, weka mayai. Tandaza vizuri. Acha yaive upande mmoja, kisha geuza vizuri upande wa pili.
 • Yai likiiva unaweza kutoa na kutenga kwa ajili ya kula.
 • Tenga chakula chako na ujirambe. Unaweza kuweka vikorombwezo unavyopenda. Binafsi huwa napendelea chakula kiwe na rangi inayovutia. Hapa nimeweka pilipili hoho, chachandu ya embe, mchuzi mzito wa supu ya kuku na pilipili pamoja na mayonaisse. Uhondo si mchezo.

20141218_202808

20141218_203527


MAPISHI YAPENDWAYO

Supu ya kuku
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.