Tambi na nyama ya kusaga

Urahisi wa kuandaa na utamu wake ni baadhi tu ya sababu za kukufanya uandae chakula hiki. Ni maalum kwa mlo mwepesi na wenye kukupa ladha. Jirambe na utofauti wa mapishi ya tambi.

Mahitaji

 • Tambi
 • Pilipili manga
 • Chumvi
 • Blueband
 • Nyama ya kusaga
 • Kitunguu maji vikate vipande vidogo sana
 • Bilinganya kata vipande vidogo
 • Pilipili hoho
 • Pilipili kali 
 • Nyanya 2 
 • Nazi
 • Tangawizi
 • Karoti
 • Royco
 • Curry powder

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Bandika sufuria, weka maji na chumvi. Ongeza pilipili manga iliyosagwa.
 • Maji yakichemka weka tambi, ziache mpaka ziive. Zichuje maji yote yaishe.
  MUHIMU: Uivishaji wa tambi unatofatiana. Kama unapenda matokeo mazuri ya tambi zisizokuwa kama uji, ni vizuri kuweka tambi kwa muda mfupi kwenye maji na kuzitoa kabla hazijaiva kabisa ili ziweze kuiva vizuri unapoendelea kupika na viungo vingine. Hivyo basi, unaweza kuzitoa kwenye maji dakika 1 au 2 kabla ya muda ulioshauriwa (Mara zote kuna maelekezo ya muda wa kupika au kuloweka tambi kwenye mfuko wake wa kuhifadhia, soma vizuri).
 • Bandika sufuria jikoni, weka blueband ikichemka weka tambi. Changanya vizuri na blueband, weka tena pilipili manga koroga vizuri kisha ipua.
 • Bandika sufuria jikoni. Weka nyama, chumvi, tangawizi na vitunguu saumu. Koroga mchanganyiko vizuri.
 •  Weka maji ya moto pale unapoona nyama inakauka. Hakikisha nyama inaiva vizuri, ipua weka pembeni.
 • Weka sufuria nyingine jikoni, weka mafuta, chumvi kidogo na kitunguu maji. Weka pilipili kali, weka bilinganya, na karoti. Koroga kisha weka pilipili hoho,endelea kukoroga.
 • Weka nyanya, na curry powder. Funika ili nyanya ziive kutengeneza mchuzi. Weka nyama kwenye mchanganyiko ule wa nyanya, ongeza royco. Endelea kukoroga.
 • Weka tui zito la nazi, subiri liive mpaka uone linakauka kisha ipua.
 • Chukua sahani pakua tambi weka na nyama ya kusaga pembeni. Hapo jirambe tu.

MAPISHI YAPENDWAYO

Samaki wenye sauce ya pilipili
dakika 35
Walaji: 4

Maandazi ya apple
dakika 5
Walaji: 5

Tambi za maziwa na iliki
dakika 15
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.