Tambi za mayai

Tambi ni chakula kizuri sana na rahisi kupika. Kutoka kwenye tambi tunapata madini na virutubisho mbalimbali kama protein,carbohydrate ambavyo vinatusaidia katika kujenga mwili.

Mahitaji

 • Tambi
 • Vitunguu maji
 • Carrot
 • Pilipili hoho
 • Vitunguu saumu
 • Curry powder
 • Mafuta
 • Mayai
 • Chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Washa jiko chemsha maji kisha yatie chumvi na mafuta kidogo.
 • Weka tambi kwenye maji ya moto mpaka uhakikishe zimeiva kisha zichuje
 • Chukua chombo chako chochote iwe bakuli au kikombe piga mayai uyaweke pembeni
 • Bandika sufuria jikoni weka mafuta kisha kitunguu maji ,kitunguu saumu,pilipili hoho,carrot na curry powder kaanga kwa pamoja ila zisiive sana.
 • Ongeza tambi zako geuza zichanganyikane na zile mboga carrot,pilipili hoho na vingine.
 • Weka mayai kwenye tambi kisha koroga haraka haraka hadi mayai yaive. Tafadhari usiache kukoroga mpaka uhakikishe tambi zako zimekua kavu na mayai yameiva.
 • Na hapo chakula chako kitakua tayari ushindwe tu wewe kujiramba

MAPISHI YAPENDWAYO

Mchemsho wa samaki na ndizi
dakika 20
Walaji: 4

Pilau ya mboga mboga
dakika 35
Walaji: 4

Ndizi mzuzu zilizoiva
dakika 13
Walaji: 2

Toa maoni yakoolivia adam
14:31, Thu 30 Oct 2014
Tuwekeeni mapishi ya pizza
Charlotte Misosi
06:42, Fri 31 Oct 2014
Olivia Adam, Karibu sana na asante kwa ushauri wako. Usiwe na shaka, maandalizi ya Pizza yanakuja hivi karibuni. Tembelea tena Misosi jumanne ijayo na utapata Pizza safi kabisa. Ni kwa ajili yako. Karibu sana Misosi
JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.