Tambi za maziwa na cheese

Tambi ni chakula cha haraka na rahisi kuandaa. Hizi tambi ni tamu sana na kama una mtoto hapendi kula mjaribu lazima atazipenda na kuzifurahia.

Mahitaji

  • Tambi kiasi
  • Butter iliyo na chumvi kijiko 1 cha chakula
  • Maji
  • Maziwa kikombe 1
  • Sukari vijiko 2 vya chakula
  • Cheddar cheese kijiko 1 cha chakula au zaidi kama utapenda
  • Maziwa ya unga kijiko 1 chakula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

  • Andaa tambi, washa jiko, bandika maji yakichemka weka tambi na butter acha zichemke dakika 5, epua chuja maji weka tambi pembeni.
  • Bandika sufuria weka maziwa acha yapate moto, weka tambi ziache kwa dakika 3 kisha weka cheese na sukari. 
  • Ziache dakika 2, epua ila hakikisha bado zina maziwa kisha weka maziwa ya unga koroga. Jirambe

MAPISHI YAPENDWAYO

Mkate wa boga
dakika 60
Walaji: 5

Njegere za nazi na maziwa
dakika 35
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.