Tambi za maziwa na iliki

Tambi ni chakula kitamu na rahisi kuandaa, tambi za maziwa na iliki ni tamu, mlaji anapata virutubisho mbalimbali pia utamu wa chakula hiki kitamfanya ajisikia furaha.

Mahitaji

  • Tambi nusu paketi
  • Sukari kijiko 1 cha chai
  • Chumvi kidogo sana
  • Mafuta ya kula vijiko 2
  • Maziwa nusu lita
  • Iriki ya kusaga au unga kijiko 1 cha chakula
  • Maji ya moto kikombe 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

  • Bandika sufuria jikoni, weka mafuta. Acha mafuta yapate moto kisha weka tambi, sukari, chumvi na iliki kwa pamoja. Kaanga kwa muda wa dakika 5 kwa moto mdogo ili kuzuia chakula kisiungue.
  • Weka maziwa yote huku ukiwa umepunguza moto kuepuka maziwa yasichemke na kumwagika. Acha tambi zichemke kwa muda wa dakika 7 kisha ongeza maji na koroga tambi. Endelea kukoroga mara kwa mara mpaka uone tambi zimeiva.
  • Epua na jirambe.

misosi-tambi-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Karanga za mayai
dakika 10
Walaji: 10

Tambi na nyama ya kusaga
dakika 25
Walaji: 2

Chachandu ya embe
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.