Tambi za nazi, njegere, hiliki na sukari

Unaweza kupika tambi kwa aina tofauti, na bila shaka umeshajaribu na kuonja mapishi mengi. Mapishi haya yanakuja na ladha tofauti kidogo kwa kuweka ladha ya nazi na njegere. Mie napenda sana nazi, na pia napenda tambi. Njegere hukipa chakula hiki upekee wa ladha. Kila nikiwa naandaa chakula hiki huwa natokwa na udenda. Chakula kina harufu nzuri, muonekano mzuri na ladha tamu mdomoni. Jaribu vitu tofauti kuongeza raha maishani kwako. Unaweza kula pamoja na kachumbari, nyama, samaki au kiambato chochote upendacho. Usisahau pia kuwa na kinywaji ukipendacho.

Mahitaji

 • Nazi
 • Tambi (Soma kwa makini muda ulioshauriwa kuzichemsha tambi kwenye paketi)
 • Hiliki
 • Sukari
 • Njegere 1/4 kilo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Tayarisha njegere kwa kuziosha na kuzichemsha hadi ziive.
 • Kuna nazi, kamua tui zito tu.
 • Menya hiliki kisha zitwange kwenye kinu.
 • Bandika maji jikoni. Yakichemka tumbukiza tambi.
 • Toa tambi kwenye maji dakika moja pungufu ya muda ulioshauriwa. Hii inasaidia kufanya tambi ziwe ngumu ili kuweza kuiva vizuri ukipika na tui.
 • Weka tambi kwenye chujio ili zitoe maji.
 • Bandika tui jikoni. Weka hiliki. Koroga mchanganyiko ili kupata tui laini na kuzuia lisikatike.
 • Weka njegere kwenye tui. Koroga ili ziweze kuchanganyika. Ni vizuri kama utaponda njegere ili kupata rojo tamu kwenye mchanganyiko.
 • Tui likishachemka weka tambi na sukari huku ukiendelea kukoroga taratibu hadi tui likauke na kubaki mafuta.
 • Chakula kipo tayari kuliwa

MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa broccoli
saa 1
Walaji: 4

Mchuzi wa biryani
dakika 35
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.