Tambi za sausage na kuku

Tambi za sausage na nyama ya kuku ya kupika taratibu. Ni chakula chepesi, chenye ladha na virutubisho murua kwa afya yako na familia yako.

Mahitaji

 • Sausage 2
 • Tambi
 • Tango
 • Nyanya 2
 • Minofu ya kuku
 • Tangawizi 1 imenywe na kusagwa
 • Kitunguu saumu 1 kimenywe na kusagwa
 • Pilipili manga
 • Olive Oil
 • Limao 1 lililokamuliwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Andaa kuku

Katika mapishi haya, kuku anachukua muda mrefu kiasi.

 • Pasha moto oven kwenye nyuzi 250°C kwa dakika 5 hadi 10.
 • Andaa minofu ya kuku, kata vipande vidogo. Osha na weka kwenye chombo cha kuoka kwenye oven.
 • Kamulia limao, weka kitunguu saumu na tangawizi. Changanya vizuri.
 • Weka chumvi na kisha nyunyuzia olive oil kwa juu.
 • Weka nyama kweye oven. Punguza joto hadi nyuzi 150°C kwa muda wa dakika 45.
 • Geuza nyama mara kwa mara.

Andaa tambi na sausage

Usiweke mafuta sababu yanazuia tambi kuiva vizuri

 • Kata sausage kwenye vipande vidogo

20141113_202203

 • Tunga tambi kwenye vipande vya sausage iwe kama mishikaki
 • Tenga sufuria ya maji jikoni, weka chumvi kisha weka tambi bila kuzikata.

20141113_203559

 

20141113_204328

 • Hakikisha tambi zimeingia vizuri kwenye chombo cha kupikia. Acha ziive kwa muda dakika 1 au 2  kabla ya muda ulioshauriwa kuiva (dakika 5 hadi 6 baada ya kuanza kuchemka)
 • Ipua tambi, chuja maji na weka kwenye sahani.

20141113_205336

 • Kata tango, nyanya kisha weka kwenye sahahi

20141113_205655

20141113_210228

 • Nyama ya kuku ikiiva, chaganya kwenye chakula.

20141113_210826

 • Jirambe….

MAPISHI YAPENDWAYO

Kuku wa kuoka
saa 1
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.