Tambi zenye iliki na sukari

Chakula kilichojaa wanga kama pasta kina virutubisho vingi. Uwepo wa viungo kwenye chakula hiki hufanya chakula kuwa kitamu. Lakini kazi ya viungo haiishii kwenye kuongeza utamu peke yake, bali hupunguza pia kasi ya kula. Matokeo yake pasta hukufanya ushibe haraka na kukuondolea adha ya kuvimbiwa. Pasta pia ina glycemic index ndogo, au unaweza kusema huchukua muda kumeng'enywa na kuongeza kiwango cha sukari kwenye damu, hivyo ni chakula kizuri kuliwa wakati wowote bila kuchafua moods zako.

Mahitaji

 • Tambi 500g 
 • Sukari vijiko 2 vikubwa
 • Iliki 3
 • Mafuta ya kupikia 1/4 lita (Nimetumia olive oil)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chakula hiki kinapikwa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni kukaanga tambi na ya pili ni kuchemsha tambi. Tambi hizi huchanganywa ili kupata mchanganyiko maridhawa wenye rangi tofauti na kuvutia. Ni vizuri kama utafanya vyote wakati mmoja, ila kama huna nafasi jikoni unaweza kuanza na kimoja kisha ukamalizia na kingine.

 • Anza kwa kumenya iliki. Hifadhi maganda yake, usitupe.

 • Toa tambi kwenye packet, kisha gawa kwenye makundi mawili – kundi moja tambi za kukaanga na lingine za kuchemsha.
 • Anza kuandaa kama ilivyoelezwa hapa chini. Ni vizuri kama utafanya hizi hatua kwa pamoja ili tambi zipate kuiva kwa muda mmoja.

Tambi za Kukaanga

 • Bandika sufuria au kikaango cha mafuta jikoni, acha yachemke vizuri.
 • Mafuta yakishachemka, ongeza fungu moja la tambi ulizotenga (Za kukaanga). Acha kwenye mafuta kwa muda kiasi hazi zianze kubadilika rangi. Ni vizuri kama hutoacha tambi zibadilike sana rangi kuwa za brown, maana zitaungua na kutokuwa na ladha nzuri. 
 • Epue tambi mapema kupata rangi ya wastani. Zitakuwa zimeiva vizuri tu.

Tambi za kuchemsha

 • Bandika chungu au sufuria ya maji jikoni kwa ajili ya kuandaa tambi za kuchemsha.
 • Weka maganda ya iliki kwenye maji ya moto ili kuweka harufu nzuri kwenye tambi. Baada ya dakika kama 5 unaweza kuchuja maganda ya iliki na kubaki na maji yenye harufu ya iliki.
 • Chukua kiasi cha tambi zilizosalia, weka kwenye maji ya moto, kisha ongeza sukari na iliki.
 • Subiria tambi zichemke kutokana na muda ulioshauriwa - dakika 5 hadi 7 - ili zisiwe na kiini kigumu ndani. Hapo tambi zako zitakua zimeiva.

Changanya Tambi

 • Changanya tambi za kukaanga na tambi za kuchemsha pamoja. Katika hatua hii unapata mchanganyiko wa rangi tofauti za tambi, harufu nzuri ya iliki na utamu wa sukari unamalizia.
 • Usisahau kutoa maoni kama ukishapika na kuonja ladha ya chakula hiki.

Jirambe na ladha ya maisha..! Mlo mwema.


MAPISHI YAPENDWAYO

Chicken curry
dakika 30
Walaji: 5

Butter chicken
dakika 45
Walaji: 4

Garlic chicken
dakika 60
Walaji: 4

Spicy grilled prawns
dakika 35
Walaji: 3

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.