Tembele

Tembele ni mboga nzuri sana ya majani na upikaji wake ni rahisi sana. Tembele kama mboga nyingine za majani inatusaidia kupata virutubisho mbalimbali muhimu mwilini. yanachangia huongezekaji wa damu pia huimarisha nguvu za viungo vya uzazi kwa wanaume.

Mahitaji

 • Tembele
 • Nyanya 3 zilizo iva vizuri
 • Ndimu au Limao 1
 • Carrot 1
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu maji 1
 • Chumvi
 • Mafuta
 • Pilipili mbuzi 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Chambua tembele vizuri, lioshe kwa maji mengi kisha weka kwenye ungo lichuje maji.
 • Bandika sufuria weka mafuta yakipata moto weka kitunguu mpaka kibadilike rangi kua ya kahawia kisha weka pilipili hoho koroga weka carrot.
 • Koroga kwa muda mchache kisha weka nyanya hakikisha nyanya zimeiva vizuri, funika kwa muda kama dakika tano ili uzipe nafasi nyanya kuiva vizuri.
 • Funua koroga ukiona nyanya zimeiva kamulia ndimu au limao koroga ili ndimu ishike kwenye viungo vizuri.
 • Tupia pilipili kuongeza radha ila haina ulazima sana ni kipendeleo cha mpishi kueka au asiweke.
 • Chukua tembele liweke ndani ya sufuria ligeuze geuze ili lichanganyikane na viungo kisha funika kidogo kama dakika tano, funua angalia kama tembele limeiva.
 • Ukiona bado halijaiva vizuri ongeza maji kidogo sana kama mills tano kisha weka chumvi ufunike.
 • Funua onja kama chumvi imeshika vizuri na tembele limeiva inavyotakiwa, hapo na uhakika tembele litakua tayari kwa kuliwa.
 • Hapo sasa jirambe kwa nafasi.

MAPISHI YAPENDWAYO

Kamba wenye mboga za majani
dakika 15
Walaji: 2

Mapishi ya ndegu kwa watoto
dakika 60
Walaji: 1

Dagaa wa nazi na karanga
dakika 15
Walaji: 4

Toa maoni yakodiana magasi
09:18, Wed 22 Jul 2015

Mko vizuri sana jaman hongereni sana kwa elimu yenu jaman.

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.