Thiep – Pilau la nyanya toka Afrika Magharibi

Haya ni moja ya mapishi toka afrika magharibi niliyowahi kuonjeshwa na rafiki yangu wakati wa pilika za kusafiri huku na kule. Mie napenda kujaribu vyakula vya jamii tofauti - ndio maana ya utamu wa maisha. Hili pilau linaonekana kama lilivyo la Kitanzania lakini lina utamu wake wa kipekee. Chakula hiki nimepika na meat balls, lakini unaweza kutumia pia nyama ya ng’ombe ya kawaida. Tahadhari ulimi – usije kujing’ata ukadhani ni chakula.

Mahitaji

 • Nyanya maji 4
 • Bilinganya 1
 • Mchele kilo 1
 • Mafuta ya kula
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu maji 1
 • Chumvi kijiko cha chai 1
 • Pilipili manga
 • Kitunguu swaumu
 • Nyama ya kuku au samaki au Meat ball

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Recipe by Isatou Keita

 • Weka mafuta ya kula kwenye sufuria na acha yapate moto.
 • Weka meat balls kwenye mafuta. Geuza geuza ili kuwezesha iive vizuri. Acha zichemke hadi ziive vizuri. Itachukua kama dakika 15.
 • Osha kisha kata bilinganya, pilipili hoho na vitunguu vipande vidogo vidogo.
 • Kata nyanya na kata vipande vidgo vidogo (unaweza pia kuziponda kwa kutumia blender ili kupata rojo nzuri au tumia nyanya ya kopo – ni chaguo lako. Pia unaweza kupika sauce ya nyanya ili iive kabla ya kuchanganya na wali)
 • Meat balls zikiiva, changanya pilipili hoho, vitunguu, nyanya na bilinganya pamoja. Acha vikaangike kwa pamoja kwa muda wa dakika 15.
 • Mchaganyiko wako ukishachemka, anza kuandaa mchele.
 • Toa vitu vyote kwenye sufuria iliyoko jikoni weka kwenye chombo tofauti. Usiipue sufuria, acha soup ilikolea nyanya na weka mchele. Ongeza maji kiasi kutokana na wingi wa mchele na kisha acha mchanganyiko uchemke kwa muda hadi mchele uive vizuri. Hapo maji yatakuwa yamekauka. Na mchele utakuwa tayari.
 • Changanya wali na mchanganyiko wa nyama na mboga za majani ulizoweka pembeni. Koroga ili kupata mchanganyiko ulio sawia.
 • Acha mchanganyiko jikoni kwa muda wa dakika 10 ili kupata kuiva vizuri kwa mboga na mchele.
 • Hiki chakula kinaliwa bila mboga, maana ni pilau linalojitosheleza. Andaa gudulia lako la maji na ujirambe. Tahadhari tu usijing’ate kutokana na uhondo utaoupata.

Enjoy chakula chako.  Washirikishe na wale uwapendao wapate kujiramba na ladha ya maisha

 


MAPISHI YAPENDWAYO

Wali wa nazi na maziwa
dakika 10
Walaji: 2

Mapishi ya tambi na kamba
dakika 20
Walaji: 2

Maandazi ya Mayai na Maziwa
dakika 20
Walaji: 4

Samaki wa kupaka
dakika 25
Walaji: 2

Toa maoni yakoBrionah Baraka Mohamed
10:14, Mon 26 Jan 2015

Chakula hiki nikitamu sana hongera sana dada yangu

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.