Togwa

Kila jamii ina aina yake ya utengenezaji wa togwa hivyo unaweza kuendelea nayo au ukajifunza njia mpya. Zingatia usafi kwenye utengenezaji wa togwa

Mahitaji

  • unga wa mahindi
  • Maji mililita125
  • Unga wa kimea cha mtama(mtama ulioteshwa ukaanikwa ukaenda kusagwa) nusu kikombe cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

  • Pika uji mzito kwa kutumia unga wa mahindi.
  • Uji ukiiva, epua na uache upoe hadi uwe wa vuguvugu.
  • Koroga unga wa kimea kwenye maji kisha weka kwenye uji wenye ujazo wa lita mbili na nusu.
  • Koroga mpaka kimea kichanganyikane vizuri na uji na kua mwepesi,
  • Funika na acha togwa ichachuke usiku kucha au kwa masaa 12.
  • Unaweza pia ukampa mtoto pale tu baada ya kupika ikipoa mana ina faida nyingi mwilini.
  • Togwa inaweza kukaa siku nzima bila kuharibika. sasa unaweza kujiramba na wanafamilia.

MAPISHI YAPENDWAYO

Creamy garlic potato
dakika 40
Walaji: 1

Chicken curry
dakika 30
Walaji: 5

Butter chicken
dakika 45
Walaji: 4

Garlic chicken
dakika 60
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.