Tortilla Sandwich

Tortilla sandwich imeandaliwa kwa mchanganyiko wa nyama ya ng’ombe na kuku. Mchanganyiko wa viungo na mboga za majani huifanya hii sandwich kuwa tamu na yenye harufu ya kuvutia. Unaweza kuandaa kwa ajili ya kwenda nayo ofisini, shule au picnic.

Mahitaji

 • Minofu ya kuku gramu 100
 • Minofu ya ng'ombe gramu  100
 • Pilipili manga ya unga kijiko 1 kidogo
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Pilipili hoho 1
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu saumu cha unga kijiko 1 kidogo
 • Karoti 1
 • Ndimu au limao ½ au unaweza kutumia vinegar
 • Curry powder kijiko 1 kikubwa
 • Mafuta ya kula, nimetumia mafuta ya zaituni (Olive oil)
 • Tortilla au chapati
 • Saladi, nimetumia kabichi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza viungo kutokana na unavyopenda.

misosi-tortilla-sandwich-ma

 • Andaa kuku – osha kisha kata vipande vidogo sana ili nyama iweze kuiva haraka na vizuri. Kamulia limao kisha changanya vizuri hadi nyama ienee limao. Nyunyuzia chumvi, koroa vizuri ili chumvi iingie kwenye nyama. Nyunyizia kitunguu saumu, koroga vizuri. Kisha hifadhi nyama pembeni.
 • Andaa nyama ya  ng'ombe – osha kisha kata vipande vidogo sana ili nyama iweze kuiva haraka na vizuri. Kamulia limao kisha changanya vizuri hadi nyama ienee limao. Nyunyuzia chumvi, koroa vizuri ili chumvi iingie kwenye nyama. Nyunyizia kitunguu saumu, koroga vizuri. Kisha hifadhi nyama pembeni.
 • Andaa pilipili hoho, kitunguu maji, kabichi na karoti. Menya kisha kata vipande vidogo kwa karoti na kitunguu. Pilipili hoho na Kabichi kata vipande virefu na vipana. Vitapendeza zaidi kwenye sandwich.
 • Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto sana. Weka mafuta kiasi. Acha hadi yapate moto. Weka nyama ya kuku, tandaza vizuri. Acha iive kwa dakika 5 kisha geuza ili iive vizuri upande wa pili. Endelea kugeuza mara kwa mara ili nyama iive na maji yakauke. Nyama ikiianza kubadilika rangi, weka pilipili manga koroga vizuri. Baada ya dakika 2 toa nyama weka kwenye chombo safi pembeni.
 • Rudia hii hatua kwa nyama ya ng'ombe, hakikisha imeiva vizuri.
 • Weka kikaango jikoni, kikipata moto weka mafuta ya kula kisha weka kitunguu maji. Kaanga vizuri hadi kianze kubadilika rangi. Weka pilipili hoho na karoti, koroga vizuri. Baada ya dakika 3 weka nyama ya kuku na ng'ombe. Koroga pamoja vizuri. Vikichanganyika vizuri, weka curry powder. Koroga vizuri hadi curry powder iendee kwenye nyama na mboga za majani vizuri. Kisha epua weka pembeni.
 • Andaa tortilla au chapati, pamoja na sauce unazotumia kwenye kula sandwich kisha tenga vizuri chakula na ujirambe.

misosi-tortilla-sandwich-0


MAPISHI YAPENDWAYO

Samaki wa mchuzi wa nazi
dakika 15
Walaji: 5

Mapishi ya spinach
dakika 18
Walaji: 3

Mapishi ya pilau la kuku
dakika 25
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.