Ugali, nyama ya kusaga na spinach

Nyama ya kusaga ikichanganywa na mboga za majani ni chakula kinachotoa virutubisho murua kwa mwili. Mchanganyiko wa spinach na nyama ya kusaga kwa kula na ugali ni chakula safi sana kula, hasa wakati wa mchana kwa kuhisi kushiba kwa muda mrefu zaidi.

Mahitaji

 • Unga ¼ kilo

Kwa spinach

 • Spinach
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Maziwa vijiko 100mls
 • Tui zito la nazi, 100mls
 • Kitunguu
 • Pilipili hoho
 • Mafuta ya kula, vijiko 2 vikubwa

Kwa nyama ya kusaga

 • Kitunguu saumu kijiko 1 kidogo
 • Tangawizi 1
 • Kitunguu saumu kijiko 1 kidogo
 • Chumvi
 • Nyama ya kusaga
 • Mafuta ya kula
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuongeza au kupunguza viungo kutokana na unavyopendelea.

nyama-misosi

Andaa nyama ya kusaga

 • Andaa nyama kwa kuiwekea viungo – tangawizi, pilipili manga, kitunguu saumu na chumvi. Hifadhi pembeni ili viungo vipate kuingia vizuri kwenye viazi.
 • Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka mafuta kidogo sana, kisha weka nyama, kaanga vizuri. Geuza upande mmoja na mwingine hadi nyama iive vizuri na kuacha kutoa maji maji. Toa na weka pembeni.

Andaa spinach

 • Andaa kitunguu, pilipili hoho. Kata vipande vidogo hifadhi pembeni.
 • Andaa spinach, osha kisha hifadhi vizuri pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni kwenye moto mkali. Acha sufuria ipate moto, weka mafuta ya kula. Weka spinach. Koroga vizuri kisha funika na mfuniko. Acha kwa dakika 1 kisha koroga halafu toa hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni, acha ipate moto vizuri. Unaweza kutumia sufuria uliyotumia kupikia spinach. Weka mafuta, weka kitunguu maji, koroga vizuri. Weka kitunguu saumu na pilipili manga na chumvi. Koroga vizuri. Weka pilipili hoho, koroga vizuri. Acha kwa dakika 2 vichemke pamoja.
 • Weka spinach, koroga vizuri. Hakikisha moto ni mkali. Weka tui la nazi, koroga hadi tui lianze kuchemka. Weka maziwa, koroga vizuri. Acha ichemke kwa dakika 3 kisha epua.
 • Mboga yako iko tayari kuliwa.
 • Andaa ugali, jirambe pamoja na mchanyiko wa mboga zako. Unaweza kuongeza chachandu, pilipili na vingine ili kuongeza ladha kwenye chakula chako.

ny2ama_misosi


MAPISHI YAPENDWAYO

Mille feuille pastry
dakika 25
Walaji: 6

Sambusa za limao na asali
dakika 30
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.