Ugali wa muhogo na mlenda

Kwa kawaida ni ugali wa muhogo, watani zangu wa jadi wazigua wanaita bada. Ni chakula halisi cha makabila tofauti ya kitanzania. Chakula kinashibisha na kina virutubisho vingi. Ni maalumu kwa wale wanaopenda kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu, lakini vizuri pia kwa wale wanaopenda kuonja chakula tofauti chenye ladha halisi.

Mahitaji

 • Unga wa muhogo ½ kilo
 • Maji
 • Sufuria ya kupikia maji
 • Nyanya chungu
 • Bamia
 • Nyanya maji
 • Kitunguu
 • Karoti
 • Pilipili hoho
 • Mafuta ya kupikia

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 

 • Ni vizuri kuanza kuandaa mboga, andaa kama maelezo haya yanavyoelekeza.
 • Ukimaliza kuandaa mboga andaa ugali wa muhogo kwa kubandika sufuria ya maji jikoni ikiwa na maji kiasi. Subiria hadi yachemke.
 • Maji yakichemka, ongeza unga wa muhogo unaotosha kusonga ugali na funika sufuria kwa dakika chache. Usikoroge maana ugali wa muhogo haupikiwa kama ugali wa sembe.
 • Baada ya dakika 3 anza kusonga. Ugali utakuwa unavutika, ni kawaida. Songa vizuri hadi unga wote uwe umepata maji na chakula kuanza kuiva.
 • Chakula kinaweza kuiva baada ya kusonga kwa dakika takribani kama 7 hadi 10 inategemea na wingi wa chakula. Hakikisha unasonga vizuri ili kupata chakula kilichoiva vizuri.
 • Chakula kikishaiva tenga pamoja na mboga na uanze kujiramba.

MAPISHI YAPENDWAYO

Sambusa za nyama
dakika 15
Walaji: 10

Macaroni ya cheese
dakika 20
Walaji: 3

Peanut butter cookies
dakika 10
Walaji: 5

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.