Uji wa mchele, umechanganywa boga na karoti

Chakula hichi ni kizuri kwa mtoto kuanzia miezi 7 na kuendelea. Mtoto anapata virutubisho muhimu kwenye chakula hiki. Brown rice ni mzuri sana kuliko mchele mweupe

Mahitaji

 • Mchele wa brown robo
 • Boga (butternut) vipande 2
 • Mafuta ( butter) kijiko 1
 • Karoti 3
 • Ladha ya strawberry nusu kijiko
 • Maziwa ( formula au breast milik)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Safisha mchele, bandika jikoni weka chumvi na maji mengi. Usiweke karoti na boga mwanzoni, sababu vitaiva kabla mchele na vitarojeka, virutubisho muhimu vitapotea.
 • Ukikaribia kuiva weka karoti na boga koroga. 
 • Weka butter, funika mpaka uive. Hakikisha maji yamebaki kidogo sana.
 • Ongeza ladha yoyote uliyonayo mimi nimeweka ladha ya strawberry koroga vizuri.
 • Hakikisha umechanganyikana vizuri na umeiva. Ipua.
 • Andaa chombo cha kusagia (blender), weka chakula ongeza maziwa saga.
 • Uwekaji wa Maziwa unategemea na uzito wa chakula unaotaka. 
 • Weka kwenye bakuli, mpe mtoto ale, pia tunza kwenye jokofu( freezer) kama kitabaki. 
 • Hapo utakua umemaliza.

MAPISHI YAPENDWAYO

Tambi na nyama ya kusaga
dakika 25
Walaji: 2

Chachandu ya embe
dakika 15
Walaji: 4

Bagia za kunde
dakika 7
Walaji: 4

Maandazi ya Vanila na Nazi
saa 1
Walaji: 15

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.