Viazi na meatballs za nazi

Chakula rahisi kuandaa cha viazi na meatballs. Kinapikwa kwa nazi na maziwa. Kinaweza kuliwa na mkate au wali,.

Mahitaji

 • Meatballs 8
 • Nazi ½
 • Maziwa ya mgando 1/8 lita
 • Karoti 1
 • Kitunguu maji 1
 • ½ kijiko cha chai cha chumvi
 • Kijiko 1 cha kitunguu saumu
 • Pilipili hoho ya kijani ½
 • Pilipili hoho nyekundu ½
 • Nyanya 4

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya viazi, osha na kisha kata vipande vidogo vidogo. Bandika jikoni na maji ya kutosha. Ongeza chumvi na funika vipate kuchemka, takribani dakika 10 hadi 15.
 • Injika chungu kwenye jiko tofauti, weka mafuta ya kula mengi na acha yapate moto.
 • Andaa viungo yako – kitunguu, pilipili hoho, nyanya, karoti na kitunguu saumu.
 • Mafuta yakipata moto, weka meatballs zako na zigeuze kila baada ya muda hadi ziive vizuri pande zote. Hakikisha zimeiva vizuri ndani. Kisha zitoe na weka kwenye chombo pembeni zipate kupoa.
 • Viazi vikiiva, ipua na injika sufuria jikoni. Weka mafuta na subiria yapate moto vizuri.
 • Weka kitunguu maji, koroga kiasi. Ongeza kitunguu saumu huku unaendelea kukoroga hadi vibadilike rangi na kuwa ya udongo iliyopauka.
 • Ongeza nyanya, koroga. Funika kidogo ipate kuiva na kulainika. Baada ya dakika 5 au 7 ponda nyanya na kisha ongeza viungo vilivyobaki kwa zamu – pilipili hoho, karoti, kisha tui la nazi na mwisho kabisa maziwa kidogo. Koroga na kisha funika vichemke vizuri. Bakisha tui kidogo.
 •  Sauce yako ikishaiva, ongeza viazi kwenye mchanganyiko, koroga na acha viendelee kuiva. Ongeza tui lililibaki na kisha koroga.
 • Mchanganyiko ukishaiva, weka meatballs, koroga kiasi, acha ichemke kwa dakika 4 hadi 6 kisha ipua; Usiache muda mrefu sababu nyama italainika sana na kubomoka.

Dokezo: Haya mapishi yaliandaliwa pamoja na maharage ya nazi na maziwa. Unaweza kupata maelezo yake ukibofya hapa.  


MAPISHI YAPENDWAYO

Chicken Curry
dakika 30
Walaji: 3

Cornbread yenye korosho
dakika 40
Walaji: 6

Bata wa mchuzi wenye Bizari
dakika 40
Walaji: 6

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.