Viazi na nyama ya kusaga

Chakula rahisi, kizuri na chenye kujaa wanga na protini. Unaweza kuandaa kwa muda mfupi na ukajiramba kwa raha zako.

Mahitaji

 • Viazi 4
 • Tangawizi 1
 • Kitunguu saumu kijiko 1 kidogo
 • Chumvi
 • Nyama ya kusaga
 • Mafuta ya kula
 • Pilipili manga

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

misosi-viazi-steak-hache-2

 • Andaa nyama kwa kuiwekea viungo – tangawizi, pilipili manga, kitunguu saumu na chumvi. Hifadhi pembeni ili viungo vipate kuingia vizuri kwenye viazi.
 • Menya viazi, kisha kata vipande vyembamba na vipana. Hifadhi kwenye maji. Weka chumvi kwenye maji ya viazi ili viazi vipate chumvi.

misosi-viazi-steak-hache

 • Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka mafuta ya kukaanga viazi. Weka viazi, kisha kaanga vizuri hadi viive. Ili kukaanga kwa muda mfupi, unaweza kuchemsha viazi kwa dakika chache kabla ya kukaanga. Viazi vikiiva epua na weka pembeni. Kama vina mafuta sana, hifadhi kwenye kitu ili vichuje mafuta.
 • Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka mafuta kidogo sana, kisha weka nyama, kaanga vizuri. Geuza upande mmoja na mwingine hadi nyama iive vizuri na kuacha kutoa maji maji. Toa na weka pembeni.
 • Tenga chakula na ujirambe vizuri.
 • Chakula hiki ni chepesi na kinaweza kuliwa wakati wowote.

misosi-viazi-steak-hache-2


MAPISHI YAPENDWAYO

Visheti vya vanilla na mdalasini
dakika 15
Walaji: 10

Chicken Tandoori
dakika 60
Walaji: 4

Shawarma ya kuku
dakika 15
Walaji: 2

Spring shrimp rolls
dakika 8
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.