Viazi vya chips za kuunga na nyanya

Jirambe na mapishi murua ya viazi vya kukaanga vyenye ladha mfano wa kachumbari ya kupikiwa moja kwa moja. Kwa mapishi haya lazima uwe na muda mzuri kwenye siku yako. Ni mapishi mazuri kwa usiku maana ni chakula chepesi kinachoweza kukufanya kuwa na njozi njema.

Mahitaji

 • Viazi mviringo (Ulaya) kilo 1
 • Nyanya maji (zilizoiva vizuri) 3
 • Nyanya ya kopo 1
 • Kitunguu maji 1
 • Kitunguu swaumu 1
 • Karoti 1
 • Pilipili hoho
 • Mafuta
 • Chumvi

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Menya viazi na kata kwenye vipande vidogo vidogo size unayopenda. Osha kisha hifadhi pembeni ili vikauke maji.
 • Andaa viungo – vitunguu, karoti, pilipili hoho, nyanya na vitunguu saumu – kwa kuosha na kuvikata vipande vidogo.
 • Nyunyuzia chumvi kwenye viazi.
 • Andaa kikaangio, weka jikoni na mafuta mengi kiasi.
 • Kaanga viazi kama unavyokaanga chips za kawaida. Hakikisha vimekauka vizuri.
 • Rudia hatua hii hadi umalize viazi vyote, kisha ipua kikaangio.
 • Bandika sufuria tofauti, weka mafuta na subiria yapate moto. Unaweza kutumia mafuta uliyokaangia chips.
 • Mafuta yakipata moto, weka vitunguu. Koroga hadi vibadilike rangi na kuwa kahawia.
 • Weka vitunguu swaumu huku ukiendelea koroga.
 • Weka pilipili hoho na karoti endelea kukoroga kwa dakika 1 hadi 2
 • Weka nyanya. Koroga kiasi ili kuzichanganay vizuri. Funika na mfuniko. Subiria hadi ziive.
 • Weka nyanya ya kopo. Koroga pamoja ili zichanganyike vizuri. Acha mchanganyiko uchemke hadi mchuzi ukauke.
 • Hakikisha kuwa hakuna mchuzi kabisa, kisha weka viazi vilivyokaangwa. Koroga ili kupata mchanganyiko mzuri. Acha ili ichemke kwa muda na roast likaukie kwenye viazi
 • Viazi vyako viko tayari kwa kula, jirambe

MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya pilau la kuku
dakika 25
Walaji: 5

Mapishi ya pilipili
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yako



JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.