Viazi vya mayai na kamba

Chakula rahisi na kitamu. Hiki chakula kinakupa virutubisho muhimu kwa afya yako – wanga na protini muhimu. Ni chakula kizuri kwa mlo mwepesi, hasa wa jioni.

Mahitaji

 • Kamba (prawns) gramu 100 (Tumia kiwango unachohitaji)
 • Viazi mbatata vilivyopondwa vikombe 2
 • Yai 1, pasua na vuruga vizuri
 • Mafuta ya kula
 • Limao au ndimu 1
 • Chumvi
 • Vitunguu saumu 2, vimenywe na kupondwa vizuri

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chakula hiki kinaandaliwa na viazi vilivyopondwa. Njia mojawapo ya kupata hivi viazi ni kuchemsha viazi mbatata hadi vinaiva vizuri kisha unaepua na kusaga hadi vinakuwa laini halafu unahifadhi pembeni. Hiki ndio tunatumia kama mojawapo ya mahitaji.

 • Weka viazi vilivyopondwa kwenye bakuli, acha vikae kwa muda hadi vipoe, takribani dakika 30. Weka yai na kitunguu saumu, bakisha kiasi kwa ajili ya kamba. Koroga vizuri. Tengeneza mchanganyiko wa viazi kwenye umbo la mviringo kisha weka kwenye chombo kisafi. Acha viazi vikae kwa dakika 15 kabla ya kupika.
 • Andaa kamba (prawns) kwa kutoa magamba. Osha kisha nyunyizia limao na chumvi. Weka kitunguu saumu. Acha kamba wakae kwa dakika 5 hadi 10 ili kitunguu saumu kiingie vizuri.
 • Bandika kikaango jikoni, weka mafuta. Yakipata moto weka vimpira vya viazi, acha viive hadi vibadilike rangi – itachukua dakika 3 hadi 5. Toa, hifadhi pembeni.
 • Kwenye kikaango tofauti, weka mafuta kidogo sana. Yakipata moto, weka kamba. Ivisha upande mmoja kwa dakika 2 hadi 3 kisha geuza upande wa pili. Epua na weka pembeni wachuje mafuta.
 • Ukimaliza andaa chakula ujirambe.

viazi-mbatata-prawns


MAPISHI YAPENDWAYO

Dagaa wa kuunga na nazi
dakika 18
Walaji: 2

Roast ya maini
dakika 30
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.