Viazi vya mboga mboga

Viazi hivi ni chakula kizuri na chepesi kuliwa wakati wowote. Unaweza kunywa na chai, kama chakula cha mchana au chakula cha usiku. Vizuri kabisa vinaweza kuliwa kama chakula cha pembeni kwenye milo tofuati pia.

Mahitaji

 • Viazi mviringo nusu kilo
 • Kitunguu
 • Pilipili hoho iliyokatwa vipande
 • Karoti iliyokatwa vipande vidogo
 • Pilipili manga ya unga
 • Kitunguu saumu kilichopondwa

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Leo tunaandaa viazi mviringo ambavyo vina viungo na mboga mboga. Tukimaliza vitakuwa kama hivi

20150118_160856

 • Andaa viazi kwa kuvimenya na kuvikata kwenye size ndogo halafu vioshe.
 • Bandika chungu jikoni. Weka viazi na chumvi kiasi. Acha viazi viive, lakini visiwe laini sana. Unaweza kuhesabu dakika 7 hadi 10 baada ya kuanza kuchemka na kuvitoa jikoni. Chuja maji na hifadhi pembeni.

20150118_155651

z20150118_155004

 • Bandika kikaango jikoni, weka mafuta. Weka kitunguu saumu. Koroga. Weka kituu maji. Koroga zaidi hadi viive vizuri – view laini na kuanza kubadilika rangi.
 • Weka viungo vilivyobaki - pilipili hoho na karoti. Koroga vizuri pamoja. Funika na mfuko ili viive pamoja kwa dakika 5 hadi 7. (Huhitaji kuvipika sana maana tunakaka mboga mboga zenye kupikwa kiasi ziwe na virutubisho vyake pamoja na umbo la kuvutia kwa ajili ya kula)
 • Weka viazi kwenye kikaango. Koroga ili vichanganyike vizuri kwa pamoja.
 • Nyunyizia pilipili manga kwa juu, kiasi tu inatosha. Hii ni kuipa ladha na harufu nzuri chakula chako.
 • Acha viazi viive kwa muda wa dakika 5 hadi 7. Kisha ipua na ujirambe.

20150118_160822

a20150118_160833

20150118_160927


MAPISHI YAPENDWAYO

Mapishi ya tambi na kamba
dakika 20
Walaji: 2

Maandazi ya Mayai na Maziwa
dakika 20
Walaji: 4

Samaki wa kupaka
dakika 25
Walaji: 2

Tambi za hiliki na sukari
dakika 8
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.