Vipopo

Vipopo ni chakula kinachoandaliwa kwa unga wa ngano na tui la nazi. Ni chakula kitamu sana kutokana na uwepo wa sukari nyingi. Ni vizuri kula hiki chakula mara chache, hasa baada ya kula chakula tofauti ili mwili uweze kuhimili ongezeko la sukari kwenye damu kwa ghafla. Pia ni vizuri kula vipopo mara chache inavyowezekana ili kupunguza madhara ya sukari.

Mahitaji

 • Unga wa ngano nusu kilo
 • Maji vikombe 3
 • Chumvi nusu kijiko cha chai
 • Mafuta ya kula
 • Tui la nazi zito vikombe 3
 • Iliki kijiko 1 cha chai
 • Sukari vijiko 3 vikubwa

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza kiwango cha sukari kutokana na unavyopendelea.

 • Weka maji na chumvi kwenye sufuria kisha bandika jikoni. Acha yachemke hadi yatokote. Weka unga kwenye maji yanayochemka kwa dadika 5 kisha songa kama ugali kwa kutumia nguvu kiasi maana huu unga ni mgumu tofauti na ugali wa kawaida. Songa kwa dakika 15, kisha mimina kwenye sinia.
 • Paka mafuta ya kula mikononi na kanda unga. Kata vidonge vidogo vya wastani vya duara, ukifanya hili zoezi usiweke mafuta au unga mkavu. Rudia zoezi mpaka unga uishe.
 • Ukimaliza kukanda, anika juani mpaka vikauke. Ukianika asubuhi unaweza kupika jioni. Si lazima uanike, unaweza kupika moja kwa moja.
 • Weka tui la nazi na iliki kwenye sufuria, bandika jikoni na acha vichemke hadi vitokote. Mimina vipopo kwenye sufuria yenye tui la nazi. Punguza moto, acha viive kwa dakika 30. Weka sukari huku ukikoroga.
 • Baada ya dakika 5 unaweza kuepua na kujiramba.
 • Vipopo ni vitamu sana, kula kwa kiwango kidogo na mara chache sana.

misosi-vipopo-main


Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.