Visheti vya vanilla na mdalasini

Visheti ni vitafunwa murua kwa kula na familia wakati wowote. Visheti hivi vina viungo vya kuvifanya vivutie zaidi - mdalasini, vanilla na vingine vingi. Unaweza kuongeza au kupunguza unavyopenda ili kupata ladha unayoitaka.

Mahitaji

 • Unga vikombe 4
 • Butter vijiko 4 cha chai
 • Iliki ½ kijiko cha chai
 • Baking powder kijiko 1 cha chai
 • Mdalasini ½ kijiko cha chai
 • Chumvi ½ kijiko cha chai
 • Tangawizi ya unga ½ kijiko cha chai
 • Maji kikombe 1½
 • Mafuta ya kula vikombe 3

Mahitaji ya kutengeneza shira

 • Sukari nyeupe vikombe 2
 • Maji kikombe 1
 • Rose water kijiko 1 cha chai
 • Vanilla nusu kijiko cha chai

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kuandaa visheti hivi kwa kuongeza au kupunguza unavyopenda ili kupata ladha unayoitaka.

 • Kwenye bakuli changanya unga, chumvi, iliki, mdalasini, baking powder na tangawizi. Changanya viungo vyote vichanganyikane vizuri na unga.
 • Yeyusha butter kidogo, weka kwenye unga, changanya vizuri hadi mafuta yapotee. Unaweza kutumia mikono kufanya hii, hakikisha mikono yako ni misafi. Ongeza maji kiasi kwenye unga, kisha kanda mpaka unga uwe laini na uache kunata. Ongeza maji mara kwa mara hadi unga uwe vizuri, itachukua takribani dakika 20. Unga ukishakandika vizuri, tengeneza umbo la duara kisha funga kwenye mfuko wa plastiki kisha weka kwenye container uache kwa dakika 20.
 • Kwenye chombo cha kukaangia, weka mafuta, weka jikoni yapate moto.
 • Nyunyiza unga kwenye ubao wa kusukumia unga. Weka donge la unga kwenye ubango wa kukusukumia. Tengeneza umbo la chapati, kata maumbo utakayopenda.

Ili kujaribu kama mafuta yamepata moto, weka kisheti kimoja kwenye mafuta yaliyo jikoni, kama kikizama kwa takribani sekunde kumi kabla hakijaibuka, mafuta yatakuwa yamepata moto vizuri, unaweza kuendelea kupika visheti. Kama kitaendelea kuelea, basi mafuta yatakuwa hayana joto la kutosha hivyo subiria kidogo maana mafuta yasipopata moto vizuri visheti vitaiva nje tu na ndani vitabaki vibichi.

 • Kaanga na kugeuza visheti mara kwa mara ili visishikane. Visheti vitaiva kama vitabadilika rangi, ila kuwa makini visiungue. Epua, weka kwenye bakuli vichuje mafuta. Muhimu kama utaweka visheti juu ya paper towel ili mafuta yajichuje vizuri.

KUTENGENEZA SHILA

 • Kwenye sufuria, weka sukari, rose water, maji na vanilla. Bandika jikoni lakini usikoroge.
 • Zungusha sufuria ili sukari na maji vichanganyikane. Shila itakua tayari, endapo ukishika kwenye vidole itanata.
 • Punguza moto. Weka visheti kwenye sufuria. Geuza kwa kutumia mwiko, hakikisha vimeshika sukari. Funika sufuria na mfuniko unaotosha. Zungusha sufuria ili visheti viendelee kushika sukari, viache kwa dakika 5 jikoni kisha zima jiko.
 • Hamisha visheti kwenye sinia au chombo kikubwa, acha vipoe kabisa kisha unaweza kula.
 • Unaweza kula visheti na chai, kahawa, maziwa au vitu vingine.

misosi-visheti-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Salad ya kabichi
dakika 5
Walaji: 5

Mtori wa ndizi
dakika 45
Walaji: 1

Pilipili ya maembe ya kusaga
dakika 35
Walaji: 5

Chicken with mashed potato
dakika 30
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.