Vitumbua vya iliki na nazi

Hivi vitumbua vinatumia unga wa mchele badala ya kuanza na mchele ulio kamili. Hii inarahisisha mapishi kwa punguza muda wa kuloweka na kisha kusaga mchele. Ni mapishi rahisi yanayotoa matokeo mazuri kwa ajili yako na wale uwapendao.

Mahitaji

 • Unga wa mchele kilo 1
 • Tui la nazi vikombe 2
 • Maji ya uvuguvugu
 • Sukari ½ kikombe
 • Iliki iliyosagwa kijiko 1 cha chakula
 • Unga wa ngano vijiko 2 vya chakula
 • Mafuta ya kula
 • Hamira ½ kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Kuwa huru kuongeza au kupunguza viungo kutokana na unavopendelea.

 • Changanya pamoja hadi uwe uji ulio sawia. Mimina mchanganyiko kwenye bakuli kisha funika vizuri na acha uumuke kiasi, takribani dakika 45 hadi 60. Ukiumuka weka sukari na changanya vizuri.
 • Weka chuma cha kuchomea vitumbua jikoni, moto usiwe mkali sana. Weka mafuta kidogo kwenye mashimo ya chuma cha kuchomea – kimoja baada ya kingine. Mafuta yakipata moto, pakua uji kwa kutumia upawa kisha jaza mashimo ya kukaangia vitumbua. Hakikisha kitumbua kinaiva vizuri na kukauka kabla ya kugeuza upande mwingine. Weka mafuta upande wa pili wa kitumbua, acha kikauke vizuri na kuwa na rangi ya kahawia. Toa kitumbua na weka pembeni. Rudia hatua hii hadi uji wa vitumbua uishe.
 • Unaweza kula vitumbua kwa aina tofauti – kitafunwa cha kila siku kwa chai, kwa kinywaji baridi au kama chakula cha kubeba kwenda kwenye picnic.  

misosi-vitumbua-iliki-main2


MAPISHI YAPENDWAYO

Ndizi za kuunga na nazi
dakika 20
Walaji: 2

Supu ya kuku
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.