Wali & mboga mseto

Chakula chenye mchanganyiko wa mboga tofauti – majani na zile zenye chanzo kikubwa cha protini za wanyama ni chanzo kizuri cha afya. Hiki chakula kimetumia mayai, nyama ya kusaga, spinach na kisamvu. Uwepo wa viungo vya kitunguu saumu, pilipili hoho, tangawizi n.k huzifanya hizi mboga kuvutia kwa harufu na tamu mdomoni.

Mahitaji

Kwa kisamvu

 • Kisamvu (Angalia kinachowatosha)
 • Kitunguu
 • Nyanya chungu
 • Pilipili (Hii ya kuleta harufu nzuri, siyo lazima kama unakula na watoto wasiokula pilipili)
 • Kitunguu saumu 1
 • Mafuta ya kula kijiko 1 kikubwa cha mezani (Mie nimetumia olive oil)
 • Sour cream (Maziwa ya mgando)– vijiko 4 vikubwa
 • Chumvi – kijiko 1 cha chai
 • Nazi – kikombe 1 (Changanya tui zito na jepesi. Kama hutumii nazi unaweza kutumia karanga, ingawa ladha haitokuwa kama kwenye hiki chakula)

Kwa spinach

 • Spinach
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Maziwa vijiko 100mls
 • Tui zito la nazi, 100mls
 • Kitunguu
 • Pilipili hoho
 • Mafuta ya kula, vijiko 2 vikubwa

Kwa nyama ya kusaga

 • Kitunguu saumu kijiko 1 kidogo
 • Tangawizi 1
 • Kitunguu saumu kijiko 1 kidogo
 • Chumvi
 • Nyama ya kusaga
 • Mafuta ya kula
 • Pilipili manga kijiko 1 kidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Angalizo: Kisamvu kinachukua muda sana kuandaa, ni vizuri kukiandaa mapema au siku moja kabla ili uweze kula chakula vizuri.

Andaa kisamvu

 • Andaa kisamvu – osha, kisha twanga vizuri kwenye kinu hadi kiwe laini. Kama una blender pia unaweza kukisaga kwenye blender, lakini njia nzuri zaidi ni kukitwanga. Kisha andaa kisamvu kama ilivyoelezwa hapa.

Andaa spinach

 • Andaa kitunguu, pilipili hoho. Kata vipande vidogo hifadhi pembeni.
 • Andaa spinach, osha kisha hifadhi vizuri pembeni. Bandika sufuria jikoni kwenye moto mkali. Acha sufuria ipate moto, weka mafuta ya kula. Weka spinach. Koroga vizuri kisha funika na mfuniko. Acha kwa dakika 1 kisha koroga halafu toa hifadhi pembeni.
 • Bandika sufuria jikoni, acha ipate moto vizuri. Unaweza kutumia sufuria uliyotumia kupikia spinach. Weka mafuta, weka kitunguu maji, koroga vizuri. Weka kitunguu saumu na pilipili manga na chumvi. Koroga vizuri. Weka pilipili hoho, koroga vizuri. Acha kwa dakika 2 vichemke pamoja.
 • Weka spinach, koroga vizuri. Hakikisha moto ni mkali. Weka tui la nazi, koroga hadi tui lianze kuchemka. Weka maziwa, koroga vizuri. Acha ichemke kwa dakika 3 kisha epua. Mboga yako iko tayari kuliwa. Hifadhi pembeni.

Andaa nyama ya kusaga

 • Andaa nyama kwa kuiwekea viungo – tangawizi, pilipili manga, kitunguu saumu na chumvi. Hifadhi pembeni ili viungo vipate kuingia vizuri kwenye viazi.
 • Bandika kikaango jikoni, acha kipate moto vizuri. Weka mafuta kidogo sana, kisha weka nyama, kaanga vizuri. Geuza upande mmoja na mwingine hadi nyama iive vizuri na kuacha kutoa maji maji. Toa na weka pembeni.
 • Andaa chakula, kisha jirambe na mboga zako tamu mchanganyiko

wali-nyama-mayai-misosi-poor


MAPISHI YAPENDWAYO

Chips na kuku
dakika 45
Walaji: 3

Spice potato curry
dakika 30
Walaji: 4

Spinach yenye maziwa na nazi
dakika 5
Walaji: 4

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.