Wali wa bizari na viungo

Je unahitaji kula wali wa bizari na viungo tofauti kwa ladha zaidi? Jaribu hiki chakula. Ni wali ulio na viungo vya kuamsha vionjo vyote vya ulimi, uliojaa ladha tamu ya viungo, wali ulioiva vizuri na kuchambuka. Unaweza kuongeza au kupunguza viungo kutokana na jinsi unavyopendelea.

Mahitaji

 • Mchele ½ kilo
 • Binzano ya njano kijiko 1 kikubwa
 • Vitunguu maji 2
 • Binzari nyembamba kijiko 1 chai
 • Iliki kijiko 1 kikubwa, twanga ½ na nyingine weka ikiwa nzima
 • Gram masala ½ kijiko cha chai
 • Mafuta vijiko 3 vikubwa
 • Hing kijiko 1 kidogo
 • Chumvi kijiko 1 kidogo
 • Mdalasini kijiko 1 kidogo
 • Tangawizi ya unga kijiko 1 kidogo

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Chakula rahisi kuandaa na chenye utamu wa kipekee. Unaweza kuongeza viungo unavyopenda ili kuongeza ladha ya chakula.

misosi-wali-bizari-main2

 • Andaa viungo – menya na vitunguu.
 • Weka mafuta yakipata moto, weka kitunguu maji. Angalia kisiive sana, kisha weka viungo vyote na koroga vizuri. Baada ya dakika 2, weka mchele na chumvi kisha koroga.
 • Weka maji ya moto kiasi funika, hakikisha mvuke hautoki. Punguza moto uwe mdogo sana.
 • Baada ya dakika 15, funua chakula, geuza na onja kama wali wa chini umeanza kuiva au umeiva kabisa. Ukiwa umeiva weka vijiko 3 vya maji, funika. Baada ya muda geuza.
 • Baada ya dakika 5 unaweza kuepua na kujiramba.

Unaweza kula chakula hiki mchana au usiku. Ni chakula muafaka kwa familia, lakini punguza viungo vikali kama kuna watoto wadogo wanaokula pia hiki chakula.

misosi-wali-bizari-main


MAPISHI YAPENDWAYO

Mkate wa ndizi na mayai
dakika 75
Walaji: 16

Tambi na mayai
dakika 10
Walaji: 1

Samaki wa ngano na tangawizi
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.