Wali wa kamba (prawns), viazi na sauce ya tomato toka Gambia

Mapishi ni sanaa, na maisha bila ujuzi wa mapishi huwa hayana ladha. Haya ni mapishi matamu ya mlo kamili wa chakula na mboga yake. Ni mapishi niliyoonja toka kwa watu wa Afrika ya Magharibi (Gambia na Senegal), ili kuhakikisha unapata ladha murua, nimeona ni bora kuweka kila kilichomo kwenye chakula nilichokula ili iwe rahisi kuonja ladha ilivyo murua.

Mahitaji

 • Curry powder
 • Viazi mviringo (ulaya) 5
 • Pilipili hoho 1
 • Pilipili manga (ya unga) kijiko 1 cha chai
 • Nyanya 4
 • Tango ½
 • Mafuta ya kula
 • Kitunguu 1
 • Kamba (prawns)
 • Mchele ½ kilo
 • Ndimu 1

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Recipe by Isatou Keita

Mapishi haya yanaandaliwa kwa hatua  4 kama zilivyoainishwa hapa chini.

Andaa wali

Andaa kamba

 • Toa magamba (kama umenunua wakiwa fresh) kisha osha kamba vizuri.
 • Nyunyuzia ndimu kwenye Kamba ili kuondoa shombo
 • Ongeza kitunguu saumu (kilichopondwa au kama una kilicho kama unga)
 • Ongeza chumvi
 • Hifadhi kama kwenye jokofu kwa muda, takribani dakika 10 ili viungo vipate kuingia vizuri
 • Bandika chombo cha kukaangia jikoni, weka mafuta ya kula kiasi, usijaze sana. Acha yapate moto.
 • Weka kamba kwenye mafuta. Wakaange vizuri. Geuza ili wapate kuiva vizuri.
 • Wakishaiva toa jikoni na hifadhi vizuri ili wasipoe.

Andaa viazi

 • Menya viazi na kata katikati, inategemea na ukubwa wa viazi. Viwe na size ya wastani tu.
 • Osha kisha kata carrot, pilipili hoho na kitunguu
 • Weka sufuria na maji jikoni.
 • Ongeza viazi, pilipili hoho na carrot kwenye sufuria ya maji jikoni
 • Acha vichemke kwa dakika 7 (angalia viazi visiive sana hadi kupondeka)
 • Ipua sufuria kisha chuja maji
 • Mchanganyiko uko tayari, hifadhi kwenye chombo kuzuia isipoe

Andaa sauce ya nyanya

 • Kutumia kitunguu, nyanya, andaa sauce ya kulia pembeni kama ifuatavyo
 • Weka sufuria na mafuta jikoni, acha yachemke kwa muda kiasi
 • Ongeza vitunguu kisha koroga hadi vitunguu vianze kubadilika rangi
 • Ongeza nyanya na chumvi, endelea kukoroga kwa dakika chache kisha funika ili kuacha mchanganyiko uive.
 • Baada ya dakika takribani 8 itakiwa tayari.

Pakua wali kiasi, weka viazi kiasi, weka mchuzi na ujirambe.

Kama umependa mapishi haya, usisahau kuwaeleza wale uwapendao. Share the love, be social.


MAPISHI YAPENDWAYO

Toa maoni yakobelinda
10:47, Tue 16 Dec 2014
Hongera kaka kwa somo zuri
Ahmed
15:21, Sun 15 Mar 2015

Nimependa elimu unayoitoa coz mi napenda sana vyakula vizuri but shidayangu ni moja nitafurahi sana km utanisaidia. Nikwamba vyakula navyokula malanyingi vinajirudia so nilikuwa naomba km hutojali ulitumie list ya vyakula vyakupika wiki nzima but visijirudie. Yani niwenajua leo kutapikwa chakulagani nakesho chakulagani naomba nisaidie kwahilo sipendi chakula kikarudiwa kupika please.

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.