Wali wa nazi na maziwa

Katika kuvunja miiko ya kuandaa chakula, tuko radhi kutafuta njia tofauti za kupika na kuongeza ladha kwenye mapishi yetu. Haya ni mapishi murua ya kuongeza appetite kwa mlaji.

Mahitaji

 • Mchele 1/2 kilo
 • Nasi ½ kifuu
 • Maji 1 lita (kawaida maji ni mara mbili ya mchele)
 • Chumvi ½ kijiko kidogo cha chai
 • Sour cream (au maziwa ya kawaida ¼ lita)

 

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Andaa tui la nazi kwa kutumia maji ya moto.
 • Osha mchele, ila usiloweke.
 • Bandika mchele jikoni na ongeza chumvi. Acha mchele hadi uanze kuchemka.
 • Baada ya kuanza kuchemka, ongeza tui la nazi pamoja na maziwa. Usikoroge. Acha mchanganyiko uive taratibu kwa takribani dakika 10.
 • Kabla maji hayajaanza kukauka, ongeza maziwa

Maalum kwa wale wanaotumia rice cooker :

Kama unatumia rice cooker ni rahisi zaidi kupika sababu unafanya kila kitu mara moja na unasubiri hadi chakula kiive. Kwenye hatua ya 3. Changanya kila kitu kwa pamoja – mchele, maji yenye tui la nazi, sour cream au maziwa na chumvi. Acha wali hadi uchemke na kuiva.

 •  Pindua chakula ili kiive vizuri. Kama unatumia jiko la mkaa na unapenda kupalilia chakula, ndio wakati umefika sasa.
 • Acha chakula hadi kiive kwa dakika 10 au 15.

N:B Kuna aina tofauti za mapishi ya wali, katika hili wengine wanapenda kuweka tui la nazi wakati wali umeshaiva na wengine wanapenda kuweka wakati wanaanza kupika. Chaguo ni lako. Cha msingi ni kuwa, maziwa yanatakiwa kuingia kwenye wali mapema ili kuweza kuiva na mchele. Hii inaongeza ladha na kuleta harufu nzuri ya chakula maradufu.


MAPISHI YAPENDWAYO

Mishikaki ya kupaka
dakika 30
Walaji: 4

Ugali wa muhogo na mlenda
dakika 15
Walaji: 2

Koliflawa na nyama ya kusaga
dakika 30
Walaji: 4

Toa maoni yakoevalyn nunge
13:34, Fri 08 May 2015

asante ,nahisi ndo nimeshapika,mate yananitoka .

JIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.