Wali wa viungo

Wali huu bado ulikua jikoni ila watu wameniomba niwaelezee jinsi ya kuupika.

Mahitaji

 • Mchele nusu kg
  Vitunguu maji 3
  Karoti 4 kubwa
  Mafuta vijiko 3 vya chakula
  Chumvi kijiko 1 cha chai
  Pilipili hoho 1
  Kitunguu saumu 1
  Pilipili manga nusu kijiko cha chai
  Iriki iliyosagwa nusu kijiko cha chai

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

 • Osha mchele,uache kwenye maji. Menya karoti katakata, vitunguu maji menya ukate kate.
 • Kitunguu saumu menya kiponde na pilipili hoho katakata.
 • Bandika sufuria jikoni, weka mafuta na vitunguu maji koroga kama dakika 2 weka vitunguu saumu, usiache kukoroga.
 • Weka karoto na pilipili hoho, weka iriki na pilipilimanga kisha funika. 
 • Weka mchele na chumvi, weka na maji kama kikombe kimoja na nusu cha chai. 
 • Funika maji yakikauka, usiugeuze ibanike baada ya dakika 10 uangalie, ugeuze onja kama bado una kiini ongeza maji kama vijiko 5 vya chakula. 
 • Funika ukija kuangalia utakua umeiva. Sasa jirambe.

MAPISHI YAPENDWAYO

Cream cheese pound cake
dakika 80
Walaji: 6

Chocolate Fondant Pudding
dakika 20
Walaji: 8

Koni za asali
dakika 25
Walaji: 10

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.