Wali wenye bamia, karoti na pilipili

Nilipowaza kuandaa hiki chakula sikuwa nadhani kitakuwa kizuri kama hivi. Lakini matokeo yake yalikuwa mazuri na wali ulikuwa mtamu sana. Nilichofanya ni kuongeza pilipili, nilikuwa na cayenne pepper za kijani, zenye ukali wa wastani, ili kuongeza ladha na utamu wa chakula. Uzuri wa hiki chakula ulinifanya nile bila hata mboga, maana bamia na karoti ziliweka ladha tamu iliyofanya wali uwe mtamu bila hata mboga.

Mahitaji

  • Mchele ½ kilo
  • Bamia 4
  • Cayenne pepper (Pilipili) 2
  • Chumvi
  • Karoti 1
  • Mafuta ya kula

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Niliandaa chakula hiki kwa kutumia rice cooker, lakini pia unaweza kupika kwa kutumia sufuria ya kawaida na jiko tofauti.

misosi-wali-bamia-main

  • Andaa bamia, karoti na pilipili. Menya karoti, kata vipande vidogo. Kata vikonyo na ncha za bamia kisha kata vipande vidogo. Kata pilipili kwenye vipande vidogo, Hifadhi pembeni.
  • Osha mchele, weka kwenye sufuria unayotumia. Changanya mafuta ya kula kiasi, chumvi pamoja na bamia, karoti na pilipili. Koroga vizuri ili vichanganyike pamoja. Ongeza maji yanayotosha kuivisha wali. Weka jikoni.
  • Acha wali uive hadi maji yakauke, kisha unaweza kugeuza ili wali wa juu na mboga mboga vipate kuiva vizuri. Acha kwenye hali ya joto kwa muda wa dakika 10 ili maji yakauke vizuri.
  • Epua wali na uandae na mboga uipendayo ili ujirambe.

misosi-wali-bamia-0


MAPISHI YAPENDWAYO

Pilipili ya maembe ya kusaga
dakika 35
Walaji: 5

Chicken with mashed potato
dakika 30
Walaji: 1

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.