Wali wenye nazi na maziwa

Wali wa nazi na maziwa una ladha tofauti na tamu sana. Ni chakula ambacho kinakufanya uvutiwe kula na ushibe haraka. Hivyo ni chakula kizuri kwa kula ili kupunguza kiasi cha chakula unachokula. Ukila chakula hiki pamoja na mboga za majani utasaidia kuboresha afya yako maana uwepo wa ufumwele (fiber) kwenye mboga za majani utakufanya ujihisi umeshiba muda mrefu zaidi.

Mahitaji

  • Mchele ½ kilo
  • Nasi ½ kifuu
  • Tui la nazi lita 1 (Nazi na Maji) (kawaida maji ni mara mbili ya mchele)
  • Chumvi ½ kijiko kidogo cha chai
  • Sour cream (au maziwa ya kawaida mililita 100)

Wapi kwa kupata bidhaa?

Je wewe unauza hivi vitu kwenye biashara yako? Bofya hapa kutuma maelezo ya biashara yako hapa ili uweze kuwafikia walaji wako.

Maelekezo

Unaweza kutumia rice cooker au sufuria ya kawaida kwenye kupika hiki chakula, ni upendeleo wako tu. Unaweza pia kupika wali kwa style ya rice cooker kwa kutumia sufuria ya kawaida kwenye jiko la kawaida. Mie nimetumia rice cooker, hivyo ntaelezea kutokana na nilivyofanya, ingawa haina tofauti kama utapika kawaida.

  • Andaa tui la nazi, hifadhi pembeni.
  • Kwenye sufuria, osha mchele, hakikisha unamwaga maji yote na usiuloweke. Pima tui na maji mara moja na nusu ya kiasi cha mchele kisha ongeza maziwa kiasi kidogo sana. Ongeza chumvi, koroga ili kuchanganya mchanganyiko na bandika jikoni. Acha ichemke vizuri hadi kila maji yakauke. Kuwa makini maana uwepo wa maziwa unaweza kufanya wali ukafurumia (kumwaga maji wakati wa kuchemka).

Kwa kawaida ili kupata wali ulioiva vizuri maji yanatakiwa kuwa mara moja na nusu au mbili ya kiasi cha mchele. Mfano,kwa kikombe 1 cha mchele unahitaji vikombe 2 vya maji (Au maji na tui). Ukizidisha maji wali utaiva kama uji bokoboko.

  • Maji yakishakauka punguza moto uwe wa wastani, pindua chakula ili kiive vizuri. Kama unatumia jiko la mkaa na unapenda kupalilia chakula, ndio wakati umefika sasa.
  • Acha chakula kikae kwenye moto mdogo hadi kiive vizuri kwa dakika 10 au 15.

N:B Kuna aina tofauti za mapishi ya wali, wengine wanapenda kuweka tui la nazi wakati wali umeshaiva na wengine wanapenda kuweka wakati wanaanza kupika. Chaguo ni lako. Cha msingi ni kufahamu kuwa maziwa yanatakiwa kuingia kwenye wali mapema ili kuweza kuiva na mchele. Hii inaongeza ladha na kuleta harufu nzuri ya chakula maradufu.

misosi-maziwa-nazi


MAPISHI YAPENDWAYO

Samaki wa kukaanga
dakika 15
Walaji: 4

Viazi vya mayai na kamba
dakika 15
Walaji: 2

Toa maoni yakoJIRAMBE..

Tafuta sehemu ya kula karibu yako

MISOSI AKAUNTI YAKO
Huna akaunti? Bofya hapa kujisajili.