MAPISHI

Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5918
Mapishi: dakika 45
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Nyama choma ni nzuri ukiwa unakunywa na vinywaji vikali au bia. Lakini si lazim, unaweza pia kula pamoja na chakula kikuu au kutumia kama kichangamsha kinywa unapokuwa unasogoa na rafiki au familia. Mie huwa napenda kula hii nyama kwa kachumbari ya nyanya pamoja na tango huku nikisindikizwa na chachandu na pilipili kali.
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 28002
Mapishi: dakika 20
Walaji: 3
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Ukipenda kula nyama, hapa utafurahia. Uzuri wa mapishi haya hayahitaji uzuri mwingi wala muda mrefu. Maelezo machache, matokeo yake yatakushangaza. Ukiwa umetulia nyumbani, bila ya haja ya kuwa na jiko kubwa, jaribu kupika hii nyama. Utapata kujua utamu wake halisi.
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 6705
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mapishi ya mishikaki yanayokuliwaza na kukupa raha ya maisha. Ni rahisi kuandaa, inafaa kuliwa vizuri taratibu ukiwa umepumzika nyumbani wakati unapata kinywaji cha kukupa afya na familia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5136
Mapishi: dakika 45
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Wastani
Mishikaki ni chakula kitokanacho na nyama ya mbuzi, samaki, kuku au nyama nyingine yoyote. Mishikaki ya kupika kwa kutumia viungo mbalimbali inayoweza kuliwa wakati wa chakula au kama kitafunwa na kinywaji. Utamu wake unaletwa na mchanganyiko adhimu wa viungo. Ni murua kutumia kwa kujiliwaza pamoja na familia au marafiki. Jirambe...
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4281
Mapishi: dakika 105
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kama unataka kupika kuku kwa aina moja tu ya mapishi, hii ndio namna ya kumpika. Kwa kawaida napenda kuku, lakini utamu wa kuku huyu ulizidi maelezo ya utamu. Niliona mapishi haya kwa rafiki yangu, yanilipa hamu ya kuandaa ili kuona matokeo yake. Kilichobakia ni mshangao, maana hakuna kilichobaki, kila kitu kilikuwa kinaliwa bila wasiwasi. Jaribu kuandaa mapishi haya kuwafanya wale uwapendao wajirambe hadi wajing’ate vidole.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3676
Mapishi: dakika 60
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Meat loaf ni chakula kizuri na rahisi kuandaa. Chakula hiki ni kitamu unaweza kula kwa aina yoyote ya kinywaji pia waweza kula muda wowote iwe asubuhi, mchana au usiku na familia ikakifurahia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 7445
Mapishi: dakika 120
Walaji: 5
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Kuku wa kuoka ni mtamu na utafurahia ladha yake pamoja na familia yako. Unaweza kula aina hii ya kuku kwa chips, ugali, ndizi za kuchoma au chakula chochote kile unachopendelea. Ni nzuri pia kushushia na kinywaji murua ili kuona ladha na utamu wa nyama ya kuoka.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2864
Mapishi: dakika 40
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Nguru ni aina ya samaki wa maji chumvi. Kama tunavyojua samaki wanatupatia madini ya chuma na protein. Unaweza kula na ugali, wali, mwenyewe au na chakula chochote na mkamfurahia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5984
Mapishi: dakika 60
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Keki ni chakula chenye ladha tamu sana. Unaweza kunywa na chai au kinywaji chochote kama maji, juice na soda au ukala yenyewe na bado ukafurahi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3963
Mapishi: dakika 40
Walaji: 6
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 10544
Mapishi: dakika 35
Walaji: 6
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Siri kubwa ya kutengeneza pizza nzuri ni kutumia viungo vizuri na bora kwa vipimo sahihi. Mapishi haya ni mazuri kwa mlo wa familia, chakula bora chenye virutubisho. Ni chakula kizuri kwa mlo mwepesi wa jioni.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3491
Mapishi: dakika 60
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Utamu wa hiki chakula utaujua baada ya kukila, si wa kuhadithiwa. Kwa ufupi, ni chakula rahisi kuandaa na kina afya inayotakiwa. Ni vizuri kukipika kama una muda kiasi, lakini ladha utakayoipata huwezi kuelezea
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4348
Mapishi: dakika 15
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Pizza ni chakula kizuri, chepesi na bora kula wakati wowote. Hapa kwenye hii pizza tunaweka sausage juu yake ili kuleta ladha zaidi. Unaweza kutumia sausage zozote upendazo au hata nyama kama unapendezewa zaidi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2658
Mapishi: dakika 45
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Butter chicken unaweka pia kupika mchuzi, kuchoma au kukaanga na bado familia yako wakafurahia mlo huo.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3844
Mapishi: dakika 60
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kuku wa kuunga kwa viungo tofauti. Ladha bora na utamu wa kipekee. Ukitaka kujaribu mapishi tofauti ya kuku, jaribu kuku huyu uone raha yake.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2143
Mapishi: dakika 35
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3398
Mapishi: dakika 60
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2065
Mapishi: dakika 40
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3382
Mapishi: dakika 45
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Tunapika samaki wa kuoka kwenye oven bila viungo vingi. Mapishi haya yanatumia chumvi na limao tu. Ni chakula rahisi kuandaa na pia matokeo yake ni mazuri sana. Ni vizuri kujaribu, onja na ujue ladha ya maisha
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4166
Mapishi: dakika 45
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kuna aina nyingi za mapishi ya nyama. Hapa leo tunaangalia nyama ya kuoka kwa kutumia viungo mbalimbali. Kisha tunakula nyama hii na ndizi mzuzu ambazo zimekaangwa kawaida kwenye mafuta. Karibu ujumuike nasi katika kuandaa chakula bora.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2619
Mapishi: dakika 45
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula kitamu, rahisi kuandaa na kinachoweza kuliwa wakati wowote ule. Jaribu mapishi haya na upate kujua ladha tamu ya maisha.
Na Anko Misosi
Imesomwa mara 2856
Mapishi: dakika 10
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Leo tunaandaa chakula chepesi na kitamu cha ndizi mzuzu na sausage. Hiki ni chakula chepesi na chenye ladha tamu. Ni maalumu kwa wale wanaume wanaobaki peke yao nyumbani na kuhisi uvivu wa kuandaa mlo mzuri, lakini afya na murua kwa kula wakati wa usiku maana hushibi hadi kuvimbiwa.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4870
Mapishi: dakika 45
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Tunapika samaki wa kuoka kwenye oven akiwa amechanganyika na ndizi mzuzu. Mapishi haya yanatumia viungo mbalimbali ili kumfanya samaki awe laini, wa kuvutia na ladha nzuri kwa kumla. Mie hufurahia chakula hiki maana hunipa matokeo bora kwa muda wangu nnaotumia katika kuandaa. Karibu ujumuike nasi katika kuandaa chakula bora.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4068
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Nyama ni chanzo kikubwa cha nyuzinyuzi pamoja na protini. Leo tunaandaa mapishi ya nyama ya kukaanga ikiwa na mchanganyiko wa viungo mbalimbali. Ili kukamilisha mlo wetu, tunaandaa nyama hii pamoja na ndizi mzuzu ambazo pia zimekaangwa kawaida kwenye mafuta. Karibu ujumuike nasi katika kuandaa chakula bora.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3764
Mapishi: dakika 45
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Hiki ni chakula kizuri kuandaa muda ulio na familia na kula pamoja, mida ya jioni au wakati wa vikao weekend. Ni chakula kizuri sababu ni kitamu na kimeandaliwa na viungo bora, hivyo kina afya tele. Hakikisha tu unafanya zoezi mara kwa mara
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3437
Mapishi: dakika 40
Walaji: 6
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Mkate huu umetengenezwa kwa umbo la kiwavi ili kukupa hamu zaidi ya kuula. Utengenezaji wake unahitaji mbinu chache na rahisi sana, ila matokeo yake ni mazuri na mkate unakuwa mtamu kutokana na viungo vinavyotumika. Huu mkate nimeufurahia maana ulikuwa unanipa hamu ya kuula kupita kiasi, na utamu wake umedhihirika pia. Nakupa na wewe ujionjee ili upate kula vitamu kama mie.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 90773
Mapishi: dakika 40
Walaji: 6
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Hii ni keki rahisi sana kuandaa lakini ni tamu kupita maelezo. Mapishi haya ya keki ni rahisi sana kupika na hayahitaji ufundi mkubwa sana. Unachotakiwa kufanya ni kuandaa vitu vizuri na kuacha mambo mengine yaendelee. Unaweza kuandaa keki hii kwa oven au kwa rice cooker. Jaribu kuandaa na uonje utamu wake.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2547
Mapishi: dakika 45
Walaji: 6
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Mie hupenda kutumia muda wangu wa weekend kuandaa vitu vitamu, hasa ku-bake mikate, cake, maandazi na vingine. Niliwahi kuonja huu mkate kabla ya kuuandaa, na sikuweza kujizuia, ikabidi niandae tu ili nipate kuhisi tena ile ladha tamu. Hakika familia ilifurahia na tulijiramba hasa. Ni mkate ulio bora, rahisi kuandaa na hauhitaji ujuzi mkubwa sana, bali ni mapenzi yako na muda mchache sana. Jirambe
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4489
Mapishi: dakika 60
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Samaki ni chakula kizuri sana, hasa akipikwa kwa staili kama hii ambapo anaiva kutokana na juisi yake mwenyewe ndani ya foil paper. Uzuri wa mapishi haya ni kuwa unapata mchuzi ambao unaweza kuuongeza kwenye mboga tofauti ilikupata ladha ya limao na viungo vya samaki.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3853
Mapishi: saa 1
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Napenda sana uokaji huu wa kuku, hasa wakati wa weekend. Huyu kuku aliiva vizuri, na hadi ngozi ikawa kavu kabisa. Muonekano, harufu na ladha yake vinaendana. Unaweza kupitiliza meno na ukashangaa umeng'ata mfupa wa kidole chako bika kujua.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4384
Mapishi: dakika 45
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Weekend huwa muda mzuri sana kwangu kujaribu vitu vingi, maana napata wakati wa kutosha wa kufanya mambo mengi. Weekend hii nilijaribu kuandaa mishikaki ya ng’ombe kwa kutumia oven. Sikuwa najua matokeo yatakuwaje lakini ikatokea vizuri. Kujaribu siyo vibaya, maana ndio mwanzo wa kujifunza. Unaweza pia kujaribu, mie nimefurahia sana maana niliweka sauce iliyo na viungo vingi na imefanya nyama imekuwa tamu.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3197
Mapishi: dakika 40
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kama una ulimi unaojua vitamu na vyenye afya, basi huyu ndio samaki wa kula. Unapata ladha ya viungo tofauti vyenye kukupa afya, lakini pia unapata virutubisho muhimu toka kwenye samaki. Samaki wa kuoka anaweza kuliwa kila kitu, ikiwezekana hata miba kama imeiva vizuri :) . Kazi kwako
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2156
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula hiki ni kitamu, rahisi kuandaa na kinavutia. Hisia zake unaweza kufumba macho kila unapomega kipande cha ndizi na kuingizia mdomoni. Ni raha iliyozidi kifani. Jaribu kuandaa na uone raha yake, hakika utafurahia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3061
Mapishi: dakika 40
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Unapenda chips lakini unaogopa mafuta mengi? Hapa umepata suluhisho. Hizi chips hazipikwi kwa kukaangwa na mafuta mengi, bali zinapikwa kwa kuokwa kwenye oven. Hizi chips ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma kutokana na viazi kuliwa vikiwa na maganda yake. Maganda ya viazi ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma. Cha zaidi, hivi viazi ni vitamu, vina ladha nzuri na vitakupa raha wakati wa kuvila. Jirambe.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3542
Mapishi: dakika 60
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Ulishawahi kula chicken tandoori? Huyu kuku unaweza kumla hadi mifupa, maana utamu wake unakuwa umezidi. Ni rahisi kuandaa na unaweza kula wakati wowote.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3582
Mapishi: dakika 60
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Samaki ni chakula kitamu, lakini samaki wa kupaka ni mwisho wa maelezo. Akipikwa kwa kutumia viungo bora, vyenye mchanganyiko mzuri, unapata matokeo yanayokupa raha kula chakula. Chakula ni kitu muhimu sana, hivyo lazima ufurahie kuandaa hadi kula. Huyu samaki wa kupaka ni mfano mzuri wa chakula kinachopendeza kuanzia kuandaa hadi kuliwa.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3398
Mapishi: dakika 30
Walaji: 6
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mishikaki huwa ni mitamu, je umeshajaribu mishikaki ya papai? Hii ni mishikaki inayokupa ladha zaidi kutokana na uwepo wa papai, bizari na pilipili. Nyama huwa laini, yenye harufu nzuri na kuvutia. Hii haiishii machoni tu, bali mdomoni unapata ladha zaidi kwa kuchangamsha vionjo vya ulimi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5183
Mapishi: dakika 20
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Kababs za kuku kwa maelezo rahisi na matokeo mazuri. Ni chanzo kizuri cha protini kutoka kwenye nyama ya kuku na mayai. Uwepo wa viungo unafanya kababs kuwa na harufu nzuri, zinavutia na kuleta vionjo vitamu wakati wa kula.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3751
Mapishi: dakika 55
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Kuandaa vitu vitamu, hasa kuoka mikate, cake, maandazi na vingine ni wakati murua sana kupitisha muda wangu. Niliwahi kuonja hii keki kabla ya kuuandaa, na sikuweza kujizuia, ikabidi niandae tu ili nipate kuhisi tena ile ladha tamu. Hakika familia ilifurahia na tulijiramba hasa. Ni keki iliyo bora, rahisi kuandaa na hauhitaji ujuzi mkubwa sana, bali ni mapenzi yako na muda mchache sana. Jirambe na keki ya chocolate
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5694
Mapishi: dakika 45
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Hizi chicken wings zinachovya kwenye mayai kisha kukaangwa kwa muda mfupi kwenye siagi. Baada ya kukaanga vinachovywa kwenye sauce na kisha kuokwa. Zikiiva utapata ladha tamu ya chicken wings laini na tamu.

Ongeza zaidi