MAPISHI

Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3490
Mapishi: dakika 15
Walaji: 5
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Ukipenda kula kuku wa kukaanga, basi huyu ndio anafaa. Chicken wings hizi unaweza kuzipika na kula kama kitafunwa wakati wa kupumzika na familia au wakati wa vikao muhimu na marafiki.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4142
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chips dume ni upishi tofauti wa viazi unaoweza kuandaliwa kwa viungo mbalimbali na pia kuweka vionjo utakavyo. Mie napenda kuweka ladha mbalimbali, na kama katika hili pishi niliweka mchuzi wa kuku na mayai. Matokeo yake yalikuwa ni zaidi ya mazuri, na chakula nikala kwa kufurahia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2976
Mapishi: dakika 10
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Ndizi za mchanganyiko na viazi vitamu ni chakula murua kula na kufurahia ladha tamu yenye afya. Mie nimefurahia hiki chakula maana kilikuwa chakula kilichozidi mategemeo yangu. Nilitaka kuandaa kitu rahisi lakini kitamu, matokeo yake nikapata hiki. Ni chakula rahisi sana kuandaa na hakichukui muda mrefu, hivyo ni muafaka kuandaa kwa wale wanaopenda kula vitu rahisi rahisi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2377
Mapishi: dakika 20
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Raha ya maisha ni kula vizuri, lakini raha zaidi inakuja pale unapojua kuandaa chakula kitamu, hasa kile roho inapenda. Hizi chicken wings ni tamu sana, zaidi kama unapenda viungo kwenye chakula. Nimetumia pilipili kali, unaweza pia usitumie pilipili na bado zikawa nzuri kukufanya ujing'ate ulimi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 8466
Mapishi: dakika 15
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kuna wakati unahitaji kuandaa kitu rahisi, kitamu na kinachotumia muda mfupi. Basi huyu samaki ndio chaguo mahsusi kwa wakati kama huo. Ni samaki mwenye viungo vichache lakini mtamu sana. Ni vizuri kwa kumla kwa ugali, maana huyu samaki akiiva vizuri anaweza kuliwa hadi miba.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2627
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula rahisi, kizuri na chenye kujaa wanga na protini. Unaweza kuandaa kwa muda mfupi na ukajiramba kwa raha zako.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3337
Mapishi: dakika 10
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Samaki ni chakula nikipendacho sana. Huwa napenda kuandaa samaki tofauti kwa mapishi yanayonivutia. Hii ni aina mojawapo ya mapishi ya samaki wa kukaanga nnayoyapenda. Samaki huyu unaanza kutamani harufu yake wakati wa kumkaanga hadi unapomalizia kula mwiba wa mwisho. Ni kazi kwako kujiramba na kufaidia maisha.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3943
Mapishi: dakika 7
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mayai ni chakula chepesi na chanzo kikubwa cha protini. Unaweza kula chakula hiki muda wowote maana ni rahisi kuandaa na pia kitamu kwa chakula.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4045
Mapishi: dakika 25
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Chips hizi na nyama zinaandaliwa kwa viungo ili kuvipa ladha tamu. Chips zikipikwa hadi kukauka vizuri huwa na ladha ya kipekee na harufu ya kuvutia. Nyama hii ina ladha tamu, ubora wa kipekee na ikiiva vizuri inaweza kukufanya ujing’ate vidole wakati wa kula.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5291
Mapishi: dakika 60
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mapishi haya ya nyama ya kukaanga ikiwa na viungo yanakupa matokeo mazuri ya nyama laini, tamu na yenye harufu nzuri. Kama unavyoiona inavyovutia, ndio itakavyokuwa ukiwa unaing'ata taratibu huku ikiwa inakupa utamu na ladha maridadi kabisa. Ni vizuri ukipika na kuona matokeo yake.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4401
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mapishi haya ya kuku yanakupa nafasi ya kuona ubora wa mapishi kwa mlo wa muda wowote unaopendelea. Unaweza kula chakula hiki asubuhi, mchana au jioni. Ndio ubora wa kuku aliyepikwa kwa staili hii.

Ongeza zaidi