MAPISHI

Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 14874
Mapishi: dakika 25
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Unaweza kula mboga hii pamoja na wali, ugali au kuchanganya na macaroni au tambi. Kizuri zaidi ni ladha ya kipekee unayoipata kutokana na mchanganyiko wa viungo
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 15888
Mapishi: dakika 10
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Katika kuvunja miiko ya kuandaa chakula, tuko radhi kutafuta njia tofauti za kupika na kuongeza ladha kwenye mapishi yetu. Haya ni mapishi murua ya kuongeza appetite kwa mlaji.
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 7182
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Chakula kinachokupa ladha ya kipekee kutokana na utayarishaji wake. Ni moja kati ya vyakula rahisi bali kwa mapishi haya hakika unapata ladha halisi ya mapishi ya tambi pamoja na mchanganyiko wa viungo tofauti. Ukila chakula hiki utaelewa umuhimu wa kutumia muda kujifunza aina tofauti za mapishi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 27651
Mapishi: dakika 25
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Haya ni mapishi mahsusi ya kuamsha vionjo vyako vya ulimi. Ladha ya nazi kwenye huyu samaki ni murua kabisa kuliwa kama mlo kamili nyumbani. Hii mboga inayofaa kuliwa na vitu tofauti, lakini mahsusi kwa wali wa nazi. Unaweza pia kula kwa vitafunwa mbalimbali kama chapati au maandazi. Kama kweli unapenda kujinoga na misosi ya ukweli, basi jaribu haya mapishi na kujiramba vizuri, hutojutia nafsi yako.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 25402
Mapishi: dakika 8
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula rahisi kwa kupika, lakini ladha yake ni tamu. Mchanganyiko wa rangi unakupa hamu ya kula. Unaweza kula pamoja na nyama (kuku, sausage, mbuzi, ng’ombe) au salad ili kuongeza ladha na vilevile rangi tofauti za vyakula. Ni vizuri pia kama ukila chakula hiki kwa salad ya nyanya, pilipili hoho na karoti ambayo inaongeza appetite sababu ya mchanganyiko wa rangi mbalimbali.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 10342
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kuna aina tofauti za ndizi – malindi, mkono wa tembo, bukoba, na nyingine kibao. Haya mapishi unaweza kupika aina yeyote ya hizo ndizi, ili mradi tu ziwe hazijaiva. Uwepo wa nazi kwenye hiki chakula unahakikisha uhalisia wa ladha na utamu wa kipekee. Unaweza kula hizi ndizi kama kitafunwa cha chai, chakula kamili au chakula kiambato ukiwa na chakula kingine mfano wali, tambi au ugali.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 13247
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Unaweza kupika tambi kwa aina tofauti, na bila shaka umeshajaribu na kuonja mapishi mengi. Mapishi haya yanakuja na ladha tofauti kidogo kwa kuweka ladha ya nazi na njegere. Mie napenda sana nazi, na pia napenda tambi. Njegere hukipa chakula hiki upekee wa ladha. Kila nikiwa naandaa chakula hiki huwa natokwa na udenda. Chakula kina harufu nzuri, muonekano mzuri na ladha tamu mdomoni. Jaribu vitu tofauti kuongeza raha maishani kwako. Unaweza kula pamoja na kachumbari, nyama, samaki au kiambato chochote upendacho. Usisahau pia kuwa na kinywaji ukipendacho.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 14289
Mapishi: dakika 35
Walaji: 4
Ujuzi: Kiwango cha juu
Gharama: Nafuu
Najua umeshaonja pilau, lakini hili ni Zaidi ya pilau. Ili kubadilisha mazingira na kuleta vionjo zaidi, jaribu kuandaa haya mapishi na kuwapa wale uwapendao vionjo vyenye ladha halisi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 12813
Mapishi: dakika 13
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mara nyingi tunakula ndizi mzuzu za kuchemsha, ukijaribu mapishi haya unaweza usile tena mapishi ya kawaida ya ndizi mzuzu. Utamu wake ni wa kipekee na hiki ni chakula bora, na hakina vikorombwezo vingi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 11414
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kisamvu ni mboga moja nnayoipenda kupita kiasi. Ni mboga ambayo hunipa ladha ya kipekee nikiipika na nazi halafu nakula pamoja na ugali. Huwezi kupinga kuwa mapishi haya yana upekee kwenye kukupa ladha halisi ya chakula cha kiafrika
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 18359
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Kuna mapishi tofauti ya nyama ya kusaga wengine wanaiosha wanachuja maji wengine wanachemsha mm naipika tofauti na hao.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 12867
Mapishi: saa 1
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Inawezekana umeshakula sana makande. Lakini haya ni mapishi tofauti kiasi. Katika mapishi haya tunatumia nazi na karanga. Ni chakula bora chenye ladha bora na kukupa hamu ya kujiramba. Kama mumeo huwa hashibi makande, inabidi uongeze kipimo maana utamu wake unaweza kumfanya amalize chakula cha familia nzima.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 11957
Mapishi: dakika 18
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Wastani
Dagaa, chanzo cha madini ya chuma mwilini. Ni chakula bora kwetu sote – wakubwa na watoto. Mapishi haya ya dagaa kwa nazi yanakupa ladha tofauti ya kukufanya kujiramba zaidi na kuongeza hamu ya kula kwako na wale uwapendao
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 10710
Mapishi: dakika 20
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Jirambe na mapishi murua ya viazi vya kukaanga vyenye ladha mfano wa kachumbari ya kupikiwa moja kwa moja. Kwa mapishi haya lazima uwe na muda mzuri kwenye siku yako. Ni mapishi mazuri kwa usiku maana ni chakula chepesi kinachoweza kukufanya kuwa na njozi njema.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 26415
Mapishi: dakika 30
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Maini ni chanzo kikubwa cha virutubisho muhimu mwilini. Roast hii hii ya maini inaweza kuliwa na wali, ugali, au pamoja na chapati. Kuna kila aina ya sababu za kula mboga hii bora na familia yako.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 10713
Mapishi: dakika 12
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Cutlets inatakiwa kupikwa na nyama laini inayoiva haraka. Hizi cutlets unaweza kuzila kwa wali au chakula kingine; unaweza pika kutafuna kwa hamu mdomoni kama wajisikia haja ya kula kitu kitamu.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 11607
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mlenda ni mboga yetu cha asili. Kuna mlenda wa aina nyingi sana. Haya mapishi yanaonyesha mojawapo kati ya mlenda unayoweza kuandaa kutumia vitu rahisi – bamia na nyanya chungu, lakini ladha yake si ya kawaida. Inafaa zaidi kuliwa na ugali ukiwa wa moto na pilipili.
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 9368
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Haya ni moja ya mapishi toka afrika magharibi niliyowahi kuonjeshwa na rafiki yangu wakati wa pilika za kusafiri huku na kule. Mie napenda kujaribu vyakula vya jamii tofauti - ndio maana ya utamu wa maisha. Hili pilau linaonekana kama lilivyo la Kitanzania lakini lina utamu wake wa kipekee. Chakula hiki nimepika na meat balls, lakini unaweza kutumia pia nyama ya ng’ombe ya kawaida. Tahadhari ulimi – usije kujing’ata ukadhani ni chakula.
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 4170
Mapishi: dakika 35
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Mapishi ni sanaa, na maisha bila ujuzi wa mapishi huwa hayana ladha. Haya ni mapishi matamu ya mlo kamili wa chakula na mboga yake. Ni mapishi niliyoonja toka kwa watu wa Afrika ya Magharibi (Gambia na Senegal), ili kuhakikisha unapata ladha murua, nimeona ni bora kuweka kila kilichomo kwenye chakula nilichokula ili iwe rahisi kuonja ladha ilivyo murua.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 9926
Mapishi: dakika 12
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mboga ya kabeji ni muhimu sana inatusaidia kupata vitamins katika miili yetu na inasaidia kuimalisha afya. Chakula hiki unaweza kula kama kitoweo au unaweza kula yenyewe kama yenyewe bado ikafaa.
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 5738
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kujiramba ni haki ya kila mmoja. Ukipenda kubadilisha ladha ya misosi kwa kujaribu vitu tofauti, jaribu kula machanganyiko huu mzuri wa vyakula vyenye afya. Ni rahisi kupika na vinakufanya unashiba haswa.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 9782
Mapishi: dakika 18
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 9950
Mapishi: dakika 25
Walaji: 5
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Pilau ni mchanganyiko wa mchele na viungo mbalimbali,chakula hiki ni kitamu sana na watu hupendelea sana kupika wakati wa sherehe. Unaweza ukala pilau na kitoweo chochote kile unachopenda mfano mimi nimependa kula na njegere,kachumbali na matunda.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4859
Mapishi: dakika 0
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Napenda kula mlo mkuu huku nikikamilisha na kitindamlo kama hiki. Ni kiambato kinachoweza kukufanya upumzike dakika chache huku ubongo wako ukipata utamu na uhondo wa sukari kwa ajili ya ubongo wako kufanya kazi vizuri.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 10702
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Pilipili ni kiungo kinachompa mlaji hamu ya kula chakula,pilipili inaeza kuekwa kwenye chakula chochote mlaji atakapopenda na kufanya mlaji apende chakula chake.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3595
Mapishi: dakika 10
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mapishi haya yanakupa ladha ya kula ndizi mzuzu za kuchoma na kuchemsha wakati mmoja. Utaandaa tofauti lakini utakuja kula kwa pamoja ili kuona ladha yake.
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 11456
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chips mayai ni chakula kinachopendwa sana kwenye jamii yetu. Kama hupendi chips mayai basi bado hujala hizi. Jaribu kujiramba na mapishi tofauti ya chips mayai zenye mchanganyiko wa mboga tofauti za majani. Kuwa makini usijing’ate, maana ni tamu hakuna mfano.
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 8158
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kwa kawaida ni ugali wa muhogo, watani zangu wa jadi wazigua wanaita bada. Ni chakula halisi cha makabila tofauti ya kitanzania. Chakula kinashibisha na kina virutubisho vingi. Ni maalumu kwa wale wanaopenda kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu, lakini vizuri pia kwa wale wanaopenda kuonja chakula tofauti chenye ladha halisi.
Na Charlotte Misosi
Imesomwa mara 4986
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Unapenda kujaribu vitu tofauti? Haya ni mapishi matamu ya mexican sauce. Ni kuku au nyama unayoweza kupika kwa aina tofauti. Viungo vya mapishi haya huleta ladha na harufu nzuri na kukufanya upate utamu na raha ya kujiramba na huu msosi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2832
Mapishi: dakika 20
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula rahisi kuandaa cha viazi na meatballs. Kinapikwa kwa nazi na maziwa. Kinaweza kuliwa na mkate au wali,.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 24498
Mapishi: dakika 15
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Tambi ni chakula kizuri sana na rahisi kupika. Kutoka kwenye tambi tunapata madini na virutubisho mbalimbali kama protein,carbohydrate ambavyo vinatusaidia katika kujenga mwili.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 14673
Mapishi: dakika 45
Walaji: 6
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Biryan ni mchanganyiko wa vyakula kama mchele,nyama,mboga za majani na viungo tofauti vya chakula. chakula hiki asili yake ni India na ni kitamu sana. Biryani inataka kufanana na pilau
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 11130
Mapishi: dakika 45
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Ndizi ni chakula kitamu sana na ni rahisi kupika. Ndizi ni chanzo kizuri sana cha vitamin C, vitaminB6 na potasium. Virutubisho hivi ni muhimu sana katika mwili wa binadamu.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 7716
Mapishi: dakika 10
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Chicken fried rice ni chakula kipendwacho zaidi na watu wa jamii ya Asia. Ni moja ya vyakula vizuri kupika nyumbani sababu ni rahisi na unaweza kupika kwa kutumia kiporo cha wali. Hiki chakula ni kitamu, ni madhubuti kwa kuipa ladha tofauti familia yako. Kama unahitaji kitu tofauti, jaribu pishi hili na ujirambe na ladha ya maisha
Na Anko Misosi
Imesomwa mara 3963
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Je una kiporo cha mboga kilichobaki na unahitaji kupata mlo mtamu wa kuchanganya? Basi hiki ndio chakula murua cha kuandaa. Chakula hiki kinakupa protini, nyuzinyuzi (fiber), wanga na mafuta. Ni chakula chepesi chenye mahsusi kuliwa usiku ili kutokula chakula kingi na kukuzuia kupata usingizi mzuri.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 16164
Mapishi: dakika 25
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Urahisi wa kuandaa na utamu wake ni baadhi tu ya sababu za kukufanya uandae chakula hiki. Ni maalum kwa mlo mwepesi na wenye kukupa ladha. Jirambe na utofauti wa mapishi ya tambi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 12288
Mapishi: dakika 45
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mtori ni chakula kizuri sana kwa mtoto, humsaidia mtoto kupata madini na virutubisho muhimu mwilini vinavyomsaidia kujenga mwili.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4843
Mapishi: dakika 30
Walaji: 1
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Mashed potato with chicken ni chakula kizuri sana na radha nzuri, chakula hiki waweza kula wakati wowote na kinywaji chochote. Pia chakula hiki anaweza kula mtoto mdogo.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 6183
Mapishi: dakika 30
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula hiki ni kizuri kwa mtoto, mana ni cha asili na kina virutubisho tosha vinavyomsaidia mtoto katika ukuaji na ujengaji wa mwili.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4971
Mapishi: dakika 40
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Wastani
Chicken tandoori ni chakula kitamu sana, asili yake ni india. Kuku huyu waweza kumla mwenyewe au ukala na chakula chochote na ukafurahi
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4893
Mapishi: dakika 30
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Wastani
Chakula hiki ni kizuri kwa watoto wote ila ni vizuri kuanzia mtoto wa miezi 9 na kuendelea. Ni kitamu na mtoto atakifurahia. Usimpe mtoto chini ya miezi mana mchanganyiko huu ni mkubwa sana kwa watoto chini ya miezi 9.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4507
Mapishi: dakika 20
Walaji: 3
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Chakula hiki ni kizuri sana, kinafaa kuliwa wakati wowote na kinywaji chochote. Na mkafurahi na familia
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2925
Mapishi: dakika 10
Walaji: 5
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 19960
Mapishi: dakika 20
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Wali huu bado ulikua jikoni ila watu wameniomba niwaelezee jinsi ya kuupika.
Na Anko Misosi
Imesomwa mara 5782
Mapishi: dakika 45
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Tambi za sausage na nyama ya kuku ya kupika taratibu. Ni chakula chepesi, chenye ladha na virutubisho murua kwa afya yako na familia yako.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 37124
Mapishi: dakika 18
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3606
Mapishi: dakika 25
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
sweet and sour chicken ni rahisi kuandaa na haichukui muda mrefu,unaweza ukala wali au ukala yenyewe tu na ukafurahi. pia unaweza kutumia juice ya nanasi badala ya nanasi
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 6596
Mapishi: dakika 35
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3306
Mapishi: dakika 40
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4738
Mapishi: dakika 30
Walaji: 5
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3377
Mapishi: dakika 45
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3641
Mapishi: dakika 30
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5727
Mapishi: dakika 10
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula kitamu, rahisi kuandaa na kinachoweza kuliwa wakati wowote ule. Jaribu mapishi haya na upate kujua ladha tamu ya maisha.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4118
Mapishi: dakika 18
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Viazi hivi ni chakula kizuri na chepesi kuliwa wakati wowote. Unaweza kunywa na chai, kama chakula cha mchana au chakula cha usiku. Vizuri kabisa vinaweza kuliwa kama chakula cha pembeni kwenye milo tofuati pia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2511
Mapishi: dakika 0
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Leo tunaandaa salad, chakula chenye afya na unachoweza kula wakati wowote bila matatizo. Kama wewe si mpenzi wa nyama, unaweza kuacha kuandaa samaki na mayai na ukala chakula hiki vizuri bila matatizo.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3935
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula hiki ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma ambayo husaidia kuongea damu. Hii inatokana na kuwa maganda ya viazi yana kiwango kikubwa sana cha madini ya chuma, hivyo ni chakula murua kwa mtu anayehitaji kuongeza damu.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2976
Mapishi: dakika 15
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula hiki nimekifurahia maana kilikuwa kina ladha tofauti sababu ya kuwepo mchanganyio wa mahindi na kamba (prawns). Nimejaribu kula sweetcorn ikichanganywa na mayai pamoja na prawns. Ni mchanganyiko mmoja mzuri sana na unaweza pia kujaribu ili upate kujiramba zaidi na chakula hiki kitamu.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2711
Mapishi: dakika 60
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mapishi haya ni maalumu kwa ajili ya hii sauce ya pilipili. Ni sauce inayoweza kuliwa na kitu chochote kile na ikapendeza. Kinachonifurahisha zaidi ni ile hali ya kukufanya ujisikie hamu ya kula lakini kukushibisha mapema kutokana na ngano iliyomo ndani yake. Ni sauce nzuri sana kwa kula na vyakula
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4774
Mapishi: dakika 35
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Hii ni mboga ya mchanganyiko wa nyama na mboga za majani. Napenda kuchanganya hivi maana mboga inakuwa na ladha nzuri na pia kuwa na virutubisho murua kwa pamoja. Ni mboga yenye virutubisho vingi mfano protini na nyuzinyuzi toka kwenye nyama na pia kwenye mboga za majani.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2959
Mapishi: saa 1
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Je unafahamu kuwa broccoli ina virutubisho vingi muhimu unavyohitaji mwilini mwako ? Basi mlo huu unakula si ladha tu peke yake, bali virutubisho vyote muhimu kwa mwili wako kunawiri. Ni mlo mzuri kwa wale wasiopenda kula na kushiba sana.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4344
Mapishi: dakika 25
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Aina tatu za mapishi unayoweza kuandaa na butternut squash. Ni rahisi kuandaa na chakula ni kizuri kwa afya pia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4117
Mapishi: dakika 40
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Je unapenda ndizi? Mimi pia napenda. Niliamua kuandaa hizi ndizi ili kupata ladha ya kila kionjo nilichokitaka kwenye chakula. Hakika ni chakula kitamu kwa muonekano na kwa ladha pia. Mchanganyiko wa nazi na maziwa huzipa ndizi hizi ladha tamu zaidi. Kama hutumii nazi unaweza kutumia karanga kama kiungo mbadala na chakula kitakuwa kitamu tu.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4138
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula rahisi na kitamu. Hiki chakula kinakupa virutubisho muhimu kwa afya yako – wanga na protini muhimu. Ni chakula kizuri kwa mlo mwepesi, hasa wa jioni.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4596
Mapishi: dakika 15
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Unapenda chips? Kama ndio, basi hii ni aina ya chips itakayokupa ladha zaidi. Chips za mayai zenye viungo tofauti mie huniliwaza sana. Napenda viungo, hasa nikiandaa kwenye chakula kitamu kama hiki - fahari ya macho, ladha mdomoni na afya mwilini. Upewe nini tena maishani hapa?
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4771
Mapishi: dakika 60
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula hiki ni kitamu, utafanya mtoto afurahi na ale sana mana atapata hamu ya kula zaidi. Na pia atapata virutubisho muhimu kwa ujenzi wa mwili na afya yake.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3205
Mapishi: dakika 21
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula hiki ni kinavutia na kitamu sana, kitakufanya ufurahie siku yako vizuri. Pia mtu ambaye yupo kwenye diet anaweza kula vizuri mana chakula kimepikwa kiafya zaidi .
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5177
Mapishi: dakika 15
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Pishi hili ni tamu na ni rahisi kuandaa, utapata vionjo vya nazi na karanga kwa pamoja.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3100
Mapishi: dakika 10
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Je wewe unahitaji nini zaidi kwenye chakula? Harufu, ladha, mvuto au? Basi, chochote unachohitaji kinapatikana kwenye huu msosi. Hii nyama inapikwa kwa muda mfupi sana, lakini matokeo yake ni mazuri mno. Ni chakula muafaka kuandaa wakati wa wikiendi kama huu ili uweze kuondoa msongo wa mazawo na uchovu wa wiki nzima. Wape uwapendao ladha tamu isiyo na mfano.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5528
Mapishi: dakika 15
Walaji: 5
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Tunatumia sana limao kama kiungo cha chakula kwa kuboresha ladha , leo basi tunatumia kwa kuweka ladha zaidi kwenye vitafunwa vya limao vyenye mayai ili kunogesha ladha. Ni vitafunio vizuri kupika kwa kupata chai au kahawa.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5526
Mapishi: dakika 25
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Je unahitaji kula wali wa bizari na viungo tofauti kwa ladha zaidi? Jaribu hiki chakula. Ni wali ulio na viungo vya kuamsha vionjo vyote vya ulimi, uliojaa ladha tamu ya viungo, wali ulioiva vizuri na kuchambuka. Unaweza kuongeza au kupunguza viungo kutokana na jinsi unavyopendelea.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2694
Mapishi: dakika 15
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Hiki ni chakula chepesi, kilichojaa protini ya kutosha. Ni mlo safi kula wakati wowote ule, iwe na chai, mchana au usiku. Ni mlo mzuri zaidi kwa usiku sababu ni chakula kisicho kizito na kinakufanya ujisikie faraja baada ya kula kwa kuweza kulala vizuri bila kuvimbiwa.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5134
Mapishi: dakika 25
Walaji: 6
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Umeshakula nyama tofauti, lakini hii bado hujaionja. Viungo vilivyo kwenye nyama hii inaifanya nyama iwe laini, tamu na yenye harufu nzuri. Ni mojawapo ya vile vilivyopikwa kwa ajili ya sikukuu ya pasaka, na vilikuwa na mvuto wa kipekee.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 8947
Mapishi: dakika 15
Walaji: 10
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Visheti ni vitafunwa murua kwa kula na familia wakati wowote. Visheti hivi vina viungo vya kuvifanya vivutie zaidi - mdalasini, vanilla na vingine vingi. Unaweza kuongeza au kupunguza unavyopenda ili kupata ladha unayoitaka.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 4567
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Shawarma ni chakula maarufu chenye asili ya nchi za mashariki ya kati. Jina la shawarma lina mizizi ya kituruki likimaanisha « kuzunguka », maana mara nyingi nyama yake huwa bonge kubwa la nyama ya kusaga ambalo huivishwa taratibu kwenye jiko kwa kuzunguka. Hii ni shawarma ya kienyeji, maana huna jiko la kuzunguka, hivyo unaweza kuandaa kirahisi kama maelezo yalivyo hapa.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2982
Mapishi: dakika 60
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Rice pudding ni chakula kizuri na kitamu sana. Chakula hiki anaweza kula mtoto na mtu mzima
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2609
Mapishi: dakika 40
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula hiki ni kitamu sana pia utapata virutubisho vingi muhimu. Pia unaweza kumtengenezea mtoto ambaye anaweza kutafuna vizuri.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3577
Mapishi: dakika 15
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Nilipowaza kuandaa hiki chakula sikuwa nadhani kitakuwa kizuri kama hivi. Lakini matokeo yake yalikuwa mazuri na wali ulikuwa mtamu sana. Nilichofanya ni kuongeza pilipili, nilikuwa na cayenne pepper za kijani, zenye ukali wa wastani, ili kuongeza ladha na utamu wa chakula. Uzuri wa hiki chakula ulinifanya nile bila hata mboga, maana bamia na karoti ziliweka ladha tamu iliyofanya wali uwe mtamu bila hata mboga.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3213
Mapishi: dakika 60
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Brown rice, chanzo cha wanga, protini na virutubisho vingine vingi. Ni chakula kizuri kwa familia nzima - watoto na watu wazima. Ni chakula kizuri sababu kina virutubisho asilia vinavyokupa afya bila kukupa madhara, tofauti na michele mingine.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2734
Mapishi: dakika 35
Walaji: 6
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Pizza, chakula rahisi kuandaa unachoweza kula wakati wowote - asubuhi, mchana au usiku. Ni vizuri kuandaa siku unayotaka kula chakula na kupumzika vizuri ukiwa unaongea na familia, marafiki au wengine Ni chakula chepesi, chenye virutubisho vingi na pia ni kitamu sana. Unaweza kuongeza vitu unavyopenda kuipendezesha pizza yako. Mapishi haya yameandaliwa na @nnjosie, asante kwa kutushirikisha kwenye kujiramba na utamu wa misosi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2455
Mapishi: dakika 100
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Couscous (inatamkwa kus kus) ni chakula chenye asili ya afrika kaskazini, hasa kwenye nchi za kiarabu za sahara – Morocco, Algeria na nyingine. Ni chakula kinachopikwa kwa kutumia mvuke, chenye utamu wa kipekee na kinachoweza kupikwa kwa kuongeza viungo tofauti, kama ilivyo wali. Couscous inapatikana kwenye maduka yanayouza vyakula asili ya kiarabu na kihindi, pia unaweza kupata kwenye supermarket tofauti.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5893
Mapishi: dakika 45
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chips zilizochanganywa na kuku, chakula hiki ni kizuri na rahisi kuandaa. Radha ya chakula hiki ni nzuri sana na utafurahia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3339
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2408
Mapishi: dakika 10
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Hiki chakula ni kitamu na rahisi sana kumuandalia mtoto. Mtoto anapata virutubisho na madini mbalimbali vinavyosaidia katika ukuaji wake. Nyanya chungu zitamsaidia kumuongezea mtoto hamu ya kula.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2029
Mapishi: dakika 30
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Hii ni mojawapo ya njia za kuongeza ladha ya mapishi kwa kutumia juisi ya ukwaju. Ukwaju, kama ilivyo limao, hufanya ladha kuwa bora zaidi. Hizi ndizi zinaweza kuliwa na watu wa rika lolote – wakubwa kwa watoto. Ni chakula rahisi kuandaa na chepesi tumboni. Unaweza kula wakati wowote ule.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3749
Mapishi: dakika 15
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kuna wale wanaopenda kula burger, lakini cha muhimu ni kula chakula kinachoboresha afya yako zaidi na siyo kuharibu. Ni vizuri kama utakula burger unayoandaa mwenyewe kwa kutumia viungo bora unavyopendelea. Ni chakula chepesi, unaweza kuandaa kwa kutumia mboga za majani kwa afya zaidi, au kwa aina ya nyama unayopenda.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3874
Mapishi: dakika 15
Walaji: 6
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Viazi vya kuchovya kwenye unga wa ngano na mayai ni chakuka rahisi kuandaa na kitamu. Unaweza kula viazi hivi kwa viambato tofauti – nyama, njegere, nyama choma, kuku, ng’ombe au vyakula vingine upendeleavyo. Ni chakula unachoweza kula wakati wowote, kwa kutofautisha kiwango kutokana na muda.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3192
Mapishi: dakika 15
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chicken wraps ni chakula rahisi na chepesi kula. Mara nyingi hiki chakula kinaliwa kikiwa cha baridi. Hivyo ni chakula muafaka cha kuandaa ili kwenda kula ofisini au shuleni. Unaweza pia kuhifahi kwenye jokofu kwa muda mrefu baada ya kuandaa na kula wakati unaopenda.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2444
Mapishi: dakika 25
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Tortilla sandwich imeandaliwa kwa mchanganyiko wa nyama ya ng’ombe na kuku. Mchanganyiko wa viungo na mboga za majani huifanya hii sandwich kuwa tamu na yenye harufu ya kuvutia. Unaweza kuandaa kwa ajili ya kwenda nayo ofisini, shule au picnic.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 9435
Mapishi: dakika 25
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3108
Mapishi: dakika 10
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Tambi ni chakula cha haraka na rahisi kuandaa. Hizi tambi ni tamu sana na kama una mtoto hapendi kula mjaribu lazima atazipenda na kuzifurahia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3915
Mapishi: dakika 30
Walaji: 8
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Paella ni chakula chenye asili ya kispaniola (Spanish recipe). Chakula hiki hupikwa kwa mapishi tofauti yanayochanganya wali na mboga tofauti – mfano: nyama, sausage, na vyakula toka baharini. Kwenye paella hii tumetumia prawns, kuku, na mboga nyingine tofauti. Ni chakula kizuri kula na familia maana kina ladha tamu na afya kwa wingi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2454
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Nyama ya kusaga ikichanganywa na mboga za majani ni chakula kinachotoa virutubisho murua kwa mwili. Mchanganyiko wa spinach na nyama ya kusaga kwa kula na ugali ni chakula safi sana kula, hasa wakati wa mchana kwa kuhisi kushiba kwa muda mrefu zaidi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3788
Mapishi: dakika 35
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Roast ya nyama ya ng'ombe na viazi ni chakula chepesi na kizuri wakati wowote unaopenda kula chakula kizuri na kuridhika bila kuvimbiwa. Pata protini, madini ya chuma, vitamini na madini tofauti kwenye chakula hiki. Uwepo wa viungo unakupa ladha tamu, harufu nzuri na raha ya kila kijiko kinachoingia mdomoni kwako.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2934
Mapishi: dakika 150
Walaji: 6
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Lasagna ni chakula asili ya kiitaliano (Italian dish) ambacho huandaliwa kwa kuwekwa matabaka (layers) ya sauce ya nyama, cheese, noodles (tambi) na pasta. Mapishi haya ya lasagna ni bora kuandaa na kula na familia, hasa wakati wa weekend maana utakuwa na muda mzuri wa kuandaa na kuyapa ladha tamu.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3428
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Macaroni ni chakula cha haraka, rahisi na bora kwa afya yako. Mchanganyiko wa nyanya, viungo na njegere kwenye macaroni unakuongezea ubora zaidi kwa kukupa virutubisho zaidi. Ni chakula unachoweza kuandaa kwa muda mfupi na kula pamoja na familia.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3695
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3524
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Wali wa nazi na maziwa una ladha tofauti na tamu sana. Ni chakula ambacho kinakufanya uvutiwe kula na ushibe haraka. Hivyo ni chakula kizuri kwa kula ili kupunguza kiasi cha chakula unachokula. Ukila chakula hiki pamoja na mboga za majani utasaidia kuboresha afya yako maana uwepo wa ufumwele (fiber) kwenye mboga za majani utakufanya ujihisi umeshiba muda mrefu zaidi.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3298
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Macaroni yana njia tofauti za kuandaa. Haya ni mojawapo ya mapishi ya kukupa macaroni matamu na yenye mvuto wa kumfanya mlaji afurahie chakula. Ni rahisi na haraka, hivyo ni chakula kizuri, chenye afya na bora kuandaa kama huna muda wa mwingi wa kukaa jikoni.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2216
Mapishi: dakika 60
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Hiki ni chakula ni kitamu na bora. Utamu wake unatokana na uwepo wa viungo vizuri vilivyochanganywa na kuku. Ubora wake unatokana na uwepo wa viazi vilivyo na maganda. Maganda ya viazi yana kiwango kikubwa cha madini ya chuma, hivyo kukifanya chakula hiki kuwa kizuri kwa wale wanaohitaji madini ya chuma kwa wingi. Ni chakula chepesi kinachokupa shibe ya kukutosha muda mrefu.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 3432
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Vipopo ni chakula kinachoandaliwa kwa unga wa ngano na tui la nazi. Ni chakula kitamu sana kutokana na uwepo wa sukari nyingi. Ni vizuri kula hiki chakula mara chache, hasa baada ya kula chakula tofauti ili mwili uweze kuhimili ongezeko la sukari kwenye damu kwa ghafla. Pia ni vizuri kula vipopo mara chache inavyowezekana ili kupunguza madhara ya sukari.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2671
Mapishi: dakika 35
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Hii ni aina nyingine tofauti ya kuandaa Pizza yenye marguez, olive na pilipili. Marguez ni sausage za ng’ombe au kondoo zenye viungo mbalimbali. Ni tamu kutumia kuandaa pizza kama hii. Hii pizza ni tamu maana ina viungo mbalimbali, unapata ladha tamu na unashiba kwa muda mrefu. Hii pizza ina vitunguu, nyanya, zaituni, marguez, pilipili za kijani na mafuta ya zaituni.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2179
Mapishi: dakika 45
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kwa wale wanaopenda vitamu, hii ni aina nyingine rahisi ya kuandaa sweet and sour chicken ya kuoka – nyama ya kuku yenye viungo vinavyoifanya iwe tamu na chachu wakati mmoja. Ni nyama nzuri inayoweza kuliwa na vyakula mbalimbali au kuliwa yenyewe kama kitafunwa kikisindikizwa na kinywaji laini. Huyu kuku amewekwa ketchup, sukari, juisi ya chungwa, red wine vinegar na sweet red chili pepper sauce.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2361
Mapishi: dakika 20
Walaji: 8
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chocolate fondant pudding ni kitindamlo (dessert) rahisi sana kinachoandaliwa kwa kutumia mayai, sukari, chocolate, siagi na unga wa ngano kiasi. Unaweza kuandaa hii pudding na kuhifadhi kwenye jokofu kwa kuila baadae. Muda unaotaka kula unaipasha moto kwa dakika chache na itakuwa safi kuliwa.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 2638
Mapishi: dakika 45
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chakula chenye mchanganyiko wa mboga tofauti – majani na zile zenye chanzo kikubwa cha protini za wanyama ni chanzo kizuri cha afya. Hiki chakula kimetumia mayai, nyama ya kusaga, spinach na kisamvu. Uwepo wa viungo vya kitunguu saumu, pilipili hoho, tangawizi n.k huzifanya hizi mboga kuvutia kwa harufu na tamu mdomoni.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 5955
Mapishi: dakika 35
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mchele wa basmati unatoa matokeo mazuri sana kwenye kupikia. Pilau hili la nyama kwa mchele wa basmati linakupa matokeo mazuri. Chakula hiki ni kizuri kupika kwa familia nzima, hasa kwenye mlo wa pamoja.
Na Dadia Msindai
Imesomwa mara 9588
Mapishi: dakika 15
Walaji: 3
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Tambi ni chakula kitamu na rahisi kuandaa, tambi za maziwa na iliki ni tamu, mlaji anapata virutubisho mbalimbali pia utamu wa chakula hiki kitamfanya ajisikia furaha.

Ongeza zaidi