Charlotte Misosi

Ubungo,
Kinondoni,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Mapishi: dakika 35
Walaji: 6
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Siri kubwa ya kutengeneza pizza nzuri ni kutumia viungo vizuri na bora kwa vipimo sahihi. Mapishi haya ni mazuri kwa mlo wa familia, chakula bora chenye virutubisho. Ni chakula kizuri kwa mlo mwepesi wa jioni.
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Unapenda kujaribu vitu tofauti? Haya ni mapishi matamu ya mexican sauce. Ni kuku au nyama unayoweza kupika kwa aina tofauti. Viungo vya mapishi haya huleta ladha na harufu nzuri na kukufanya upate utamu na raha ya kujiramba na huu msosi.
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kwa kawaida ni ugali wa muhogo, watani zangu wa jadi wazigua wanaita bada. Ni chakula halisi cha makabila tofauti ya kitanzania. Chakula kinashibisha na kina virutubisho vingi. Ni maalumu kwa wale wanaopenda kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu, lakini vizuri pia kwa wale wanaopenda kuonja chakula tofauti chenye ladha halisi.
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Mapishi ya mishikaki yanayokuliwaza na kukupa raha ya maisha. Ni rahisi kuandaa, inafaa kuliwa vizuri taratibu ukiwa umepumzika nyumbani wakati unapata kinywaji cha kukupa afya na familia.
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Chips mayai ni chakula kinachopendwa sana kwenye jamii yetu. Kama hupendi chips mayai basi bado hujala hizi. Jaribu kujiramba na mapishi tofauti ya chips mayai zenye mchanganyiko wa mboga tofauti za majani. Kuwa makini usijing’ate, maana ni tamu hakuna mfano.
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kujiramba ni haki ya kila mmoja. Ukipenda kubadilisha ladha ya misosi kwa kujaribu vitu tofauti, jaribu kula machanganyiko huu mzuri wa vyakula vyenye afya. Ni rahisi kupika na vinakufanya unashiba haswa.
Mapishi: dakika 35
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Mapishi ni sanaa, na maisha bila ujuzi wa mapishi huwa hayana ladha. Haya ni mapishi matamu ya mlo kamili wa chakula na mboga yake. Ni mapishi niliyoonja toka kwa watu wa Afrika ya Magharibi (Gambia na Senegal), ili kuhakikisha unapata ladha murua, nimeona ni bora kuweka kila kilichomo kwenye chakula nilichokula ili iwe rahisi kuonja ladha ilivyo murua.
Mapishi: dakika 5
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Usipagawe kuona juisi ya moto, kama hujawahi kunywa basi jaribu hii. Huwezi kujutia. Ni kinywaji murua kwa wakati wa kupumzika jioni ukiwa unatafakari maisha. Ni kinywaji mbadala asubuhi kwa chai, maana hunywewa kikiwa cha moto na hakuna sukari inayoongezwa bali asali ambayo haina madhara mwilini. Kuwa makini maana asali huwa inakufanya upate usingizi kirahisi.
Mapishi: dakika 5
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Kula kwa afya ni muhimu, hasa pale unapokuwa unataka kula vizuri na kutotibua ratiba zako za kufanya kazi kwa ufasaha ukiwa ofisini. Salad ni chakula chepesi, kinakupa nguvu za kutosha na kuzuia adha zinazotokana na kushiba kupita kiasi. Salad hii ina nyama kiasi ambayo inaweza kukupa nguvu ziadi, hasa kwa wale wanaopenda kula nyama katika kila mlo. Jirambe na ladha ya maisha.
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Haya ni moja ya mapishi toka afrika magharibi niliyowahi kuonjeshwa na rafiki yangu wakati wa pilika za kusafiri huku na kule. Mie napenda kujaribu vyakula vya jamii tofauti - ndio maana ya utamu wa maisha. Hili pilau linaonekana kama lilivyo la Kitanzania lakini lina utamu wake wa kipekee. Chakula hiki nimepika na meat balls, lakini unaweza kutumia pia nyama ya ng’ombe ya kawaida. Tahadhari ulimi – usije kujing’ata ukadhani ni chakula.
Mapishi: dakika 35
Walaji: 4
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Maisha ni kujaribu. Na mie siachi kujaribu mapishi. Hapa nachanganya maharage na viungo viwili murua ili kuyapa ladha tofauti na ya kipekee. Nilishazoea kula maharage yanayopikwa bila nyanya wala vikorombwezo tofauti, lakini leo hii napenda zaidi maharage yenye nyanya, maziwa, nazi na juu ya yote, nimeweka karanga. Uhondo wa mboga hii hauna kifani.
Mapishi: dakika 20
Walaji: 3
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Ukipenda kula nyama, hapa utafurahia. Uzuri wa mapishi haya hayahitaji uzuri mwingi wala muda mrefu. Maelezo machache, matokeo yake yatakushangaza. Ukiwa umetulia nyumbani, bila ya haja ya kuwa na jiko kubwa, jaribu kupika hii nyama. Utapata kujua utamu wake halisi.
Mapishi: dakika 30
Walaji: 4
Ujuzi: Wastani
Gharama: Nafuu
Nilidoea mapishi haya kwa jirani, nikapagawa na nikalazimika kuyapika kwangu siku inayofuatia. Si mapishi magumu, bali ni tofauti na yale niliyozoea kuandaa kwangu hakika yamenipa raha. Ni aina ya mapishi yamezoeleka sana Afrika magharibi – najua wotu tunaunga kwa karanga, ila upishi wake niliupenda. Najua ukijaribu utayapenda, jirambe na utamu huu. Usikose kuelezea utamu uliopata ukishajiramba.
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Wastani
Supu ya kuku yenye ladha tofauti kutokana na mchanganyiko wa mboga za majani. Inaweza kuliwa na mkate, maandazi, ikiwa tupu au vingine upendavyo.
Mapishi: dakika 20
Walaji: 2
Ujuzi: Wastani
Gharama: Wastani
Chakula kinachokupa ladha ya kipekee kutokana na utayarishaji wake. Ni moja kati ya vyakula rahisi bali kwa mapishi haya hakika unapata ladha halisi ya mapishi ya tambi pamoja na mchanganyiko wa viungo tofauti. Ukila chakula hiki utaelewa umuhimu wa kutumia muda kujifunza aina tofauti za mapishi.
Mapishi: dakika 10
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Katika kuvunja miiko ya kuandaa chakula, tuko radhi kutafuta njia tofauti za kupika na kuongeza ladha kwenye mapishi yetu. Haya ni mapishi murua ya kuongeza appetite kwa mlaji.
Mapishi: dakika 25
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Unaweza kula mboga hii pamoja na wali, ugali au kuchanganya na macaroni au tambi. Kizuri zaidi ni ladha ya kipekee unayoipata kutokana na mchanganyiko wa viungo
Kama wasemavyo, mapishi ni sanaa, nikisema vingine ntakuwa nakosea. Unaweza kula chakula cha aina moja kwa watu tofauti ukahisi kama vile umekula vyakula tofauti. Leo tunaweka tovuti mbalimbali zinazoelimisha kuhusu mapishi ili upate kujifunza ladha tofauti.


Maisha ni matamu na raha ya wanaijua wale wanaofahamu siri za vyakula. Mie nakudokezea siri mojawapo - chakula bora ni muhimu kwa afya na furaha yako. Bila chakula bora, hakuna raha katika maisha yako hapa duniani.


Je huwa una kasumba ya kutopata staftahi (kifungua kinywa) kila asubuhi?


Ili kuwa na siha njema ni muhimu kula vizuri. Kula vizuri si rahisi, ingawa wengi wetu tunadhani kula vizuri ni kula chakula tunachokipenda – chips, kuku, mayai, nyama na vingine. Hii ni kasumba mbovu tu. Kula vizuri (au balanced diet) si lazima kula vyakula unavyopenda, bali kula vyakula vyenye afya na kujenga mwili wako. Njia moja mbadala ya kuhakikiasha unakula vizuri na kwa afya ni kuwa na ratiba ya wiki ya chakula. Leo tunaangalia umuhimu wa kupanga ratiba ya chakula kwa afya yako na familia yako.


Afya huanzia kwenye vitu vidogo sana, hasa vile vinavyolenga moja kwa moja afya zetu. Ukichunguza sana utagundua kuwa matatizo mengi ya kiafya hutokana na uzembe wetu tunaofanya kila siku nyumbani. Hii inawezekana ni sababu ya uvivu au kutojali tu. Leo hii naomba kugusia mambo machache muhimu ambayo ningefurahi kuyaweka bayana kuhusu afya za kaya zetu.


Wahenga wanasema nyota njema hung’ara asubuhi – mie kila asubuhi huwa ni muda muafaka wa kuanza siku yangu kwa kuzingatia afya. Kwa kawaida huwa napenda kuanza siku na chai au maji yaliyochanganywa na limao. Limao ni kitu kidogo sana lakini faida zake huwezi kuamini kama hujawahi kutumia. Leo hii naomba nikudokeze kidogo ili nawe upate kujua.


Afya ya mtu huanzia kwenye harufu ya mwili wake. Hakuna harufu inayoonyesha jinsi gani ulivyo msafi kama harufu ya kinywa. Je ulishawahi kuongea na mtu na ghafla ukajikuta unakosa hamu ya kuendelea sababu kinywa kinatoa harufu mbaya? Nafahamu kero hii inavyokuwa.


Ni amani na furaha pale matumbo yanapokuwa yamejaa. Raha zaidi inakuwa pale tunaposhiriki kikamilifu kwenye kuandaa chakula na mwisho kuonja kazi ya mikono yetu.  


Chakula ni kitu muhimu, lakini si bora chakula tu, kinachotakiwa ni chakula bora. Ni ukweli usiopingika kuwa kutokana na wengi wetu kubanwa na majukumu ya kazi na kukosa muda wa kufanya shopping ya vyakula kila wakati huwa tunaishia kula vyakula visivyo na kiwango kinachofaa. Ni muhimu kujipanga na kununua bidhaa bora kwa wakati  na  kuzihifadhi vizuri kwa akiba yako nyumbani. Dhumuni hapa ni kulinda ubora wa bidhaa zako ili kuwa na chakula bora kila wakati - kwako na familia yako.


Mafuta ya kula ni kiungo muhimu sana kwenye mapishi yetu ya kila siku. Baadhi yetu hatuwezi kuandaa chakula bila kutumia mafuta kabisa. Lakini kila mtu anafahamu madhara ya mafuta, hasa ukitumia kwa wingi na kutumia mafuta yasiyo na kiwango bora - ambayo hupatikana kwa wingi na bei nafuu zaidi. Je kuna njia gani mbadala za kupunguza matumizi haya ya mafuta? Leo hii tunaangalia njia mbadala za mafuta ya kula ili kulinda afya zetu na wale tuwapendao.

Mara nyingi kutokana na pilika za maisha, huwa hatujali tunakula nini na kila tunachonunua vina viambato gani. Si kila mtu ana muda na kasumba ya kuchunguza mafuta au bidhaa anazonunua - wengi tunaangalia gharama na upatikanaji.  Si kila mchuuzi anajali anachowauzia wateja wake, kwa hiyo afya zetu ziko mikononi kwa wale wanaotupa huduma. Je ungependa kuwa makini zaidi na unachokula?


Teknolojia inatuleta mambo mapya kila kukich. Kila kitu kinachogunduliwa huwa na uwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja, lakini kujua matumizi ya vitu vingi lazima uwe mdadisi. Misosi Team inapenda kukurahisishia maisha kwa kukupa tips muhimu kwenye anga tofauti za maisha, hasa kwenye maswala ya nyumbani na mapishi. Leo tunaangalia orodha ya matumizi ya microwave yako, maana yako mengi, na haya ni baadhi tu ya yale tunayofahamu.


Nakumbuka wakati nikiwa mdogo, nilikuwa natoka shule njaa inauma namsubiria mama arudi toka kazini ili nipate kula chakula cha mchana. Kila akiwa anafika nyumbani huanza kuuliza – " leo unataka kula nini mwanangu?". Hili lilikuwa ni swali la kwanza kuulizwa akirudi nyumbani. Nilikuwa nafarijika sana moyoni maana ilikuwa inaonyesha jinsi gani nnavyothaminiwa maana si kila mtoto alikuwa na nafasi ya kuchangia mawazo kwenye maamuzi ya vyakula nyumbani, na hasa kule uswahilini kwetu. Lakini sikuelewa kuwa lile swali lilikuwa na maana kubwa zaidi ya kutaka kujua mie napenda kula nini. Nakiri kuwa sikuwahi kufikiria kuhusu hilo hadi nilipokuwa kijana wa kuanza kujitegemea. 


Misosi ni jumuiya ya watu tunaopenda kubadilishana mawazo juu ya vitu tofauti maishani. Tunafahamu kuwa kati ya vitu muhimu kabisa kwenye maisha ni chakula. Jinsi tunavyokula na kuridhika ina umuhimu sana kwenye kutupa furaha na amani maishani. Amani kwenye maisha huanza pale tunapokula vizuri na kuridhika. Misosi Team, tunawapa watu nafasi ya kufanya haya yote kwa kuchangia mapishi, kutoa maoni yao na hata kuweka biashara zao kwa wanaouza bidhaa za nyumbani na vyakula. Sisi tunatoa fursa, wewe unachagua cha kufanya kutokana na hii fursa, hakuna kikwamo zaidi ya ubunifu wako. Na hii fursa ni kwa yeyote aliye na nia ya kuiambia jamii juu ya maisha. 

Sisi kama jamii tunapenda:

  • Kuchangia mawazo ili kujifunza zaidi kuhusu maisha, hasa mapishi na sehemu za kupata bidhaa bora
  • Kutoa nafasi ya watu wanaopenda kujumuika na watu wengine ili kuchangia yale tupendayo kwenye maisha
  • Vyakula vya aina mbali mbali ili kuweza kubadilisha ladha ya maisha kila siku.

Misosi tunawakaribisha kwenye libeneke hili ambapo utaweza kutuma mapishi, biashara na kutangaza matangazo yako bila matatizo, na ni bure kabisa.

Karibuni sana tujirambe na ladha ya maisha