Anko Misosi

Ubungo,
Kinondoni,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Mapishi: dakika 10
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Leo tunaandaa chakula chepesi na kitamu cha ndizi mzuzu na sausage. Hiki ni chakula chepesi na chenye ladha tamu. Ni maalumu kwa wale wanaume wanaobaki peke yao nyumbani na kuhisi uvivu wa kuandaa mlo mzuri, lakini afya na murua kwa kula wakati wa usiku maana hushibi hadi kuvimbiwa.
Mapishi: dakika 45
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Tambi za sausage na nyama ya kuku ya kupika taratibu. Ni chakula chepesi, chenye ladha na virutubisho murua kwa afya yako na familia yako.
Mapishi: dakika 10
Walaji: 1
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Nilikuwa na hamu ya kula chakula laini, chenye afya. Kutokana na kuwa peke yangu, hiki kilikuwa chakula mahsusi na kitamu cha kufanya usiku wangu uwe murua sana. Kizuri zaidi, sikuwa na haja ya kutumia kitu chochote cha moto, nimekula chakula hiki kwa macaroni ya baridi na maziwa ya mgando (yoghurt) baridi. Unaweza kushangaa, lakini ni afya kula chakula cha wanga cha baridi.
Mapishi: dakika 15
Walaji: 2
Ujuzi: Rahisi
Gharama: Nafuu
Je una kiporo cha mboga kilichobaki na unahitaji kupata mlo mtamu wa kuchanganya? Basi hiki ndio chakula murua cha kuandaa. Chakula hiki kinakupa protini, nyuzinyuzi (fiber), wanga na mafuta. Ni chakula chepesi chenye mahsusi kuliwa usiku ili kutokula chakula kingi na kukuzuia kupata usingizi mzuri.
Kuna wakati maishani unaweza ukawa unafikiria kuongezeka uzito, na hii ni hali ya kawaida. Mimi binafsi nimeshapita katika hali hii. Vilevile, nimeona watu waliokuwa wanatamani kuongezeka uzito, japo kidogo ili kuweza kufikia kilo wanazohitaji. Wakati mwengine hili zoezi huwa gumu kutokana na kutoelewa mbinu muhimu za kufanya vitu kwa usahihi.


Afya ni kitu muhimu sana kwenye maisha yako kama binadamu. Kuwa na afya bora ni nusu ya mafanikio. Fahamu kwamba hakuna kitu muhimu zaidi ya afya yako. Wengi wetu kujiendekeza kunatuharibia afya, matokeo yake tunashindwa kufanya kazi, tunazembea na kumalizia hela kwenye madawa na matibabu yasiyo na msingi. Kila kitu ni kwa kudra za Mwenyezi Mungu, lakini utashi wako unahusika sana katika kuiboresha au kuibomoa siha yako. Wahenga wanasema, jali afya yako ikutunze.


Kila mwanzo wa mwaka tunakuwa na malengo mengi na mipango ya kuboresha afya zetu. Ni katika kipidi kama hiki ambapo wengi tuna kasumba ya kupanga kupunguza uzito, kuboresha afya, kuongeza bidii kazini, kuboresha ujuzi, na mengineyo mengi.


Kila siku ni nafaasi nyingine ya kuleta maendeleo kwako, familia yako, na kwa taifa kwa ujumla. Waswahili wanasema nyota njema huonekana asubuhi, je unaanza siku vizuri?


Ulaji wa supu ya pweza, karanga mbichi, muhogo mbichi, mbata kwa dai kwamba vinaongeza urijali kwa wanaume kumeelezwa kuwa ni dhana potofu inayostahili kupigwa vita kwa kuwa haina uhusiano kati ya urijali wa mwanaume na virutubisho vinavyotolewa na vyakula hivyo.


Waswahili wanasema mazoea yana tabu na mara nyingi vitu tulivyovizoea hupoteza thamani yake hadi pale vinapopotea. Hivyo, ili kuthamini kile ulichonacho na kukipa heshima yake, mie nashauri ujaribu kufanya vitu tofauti na mazoea yako ya kila siku ili kujua ubora wa kile ulichonacho. Hii itakufanya uzidi kuthamini ulivyonavyo na hasa kukupa ladha zaidi na maisha yako.


Je wewe unapenda kiporo? Basi leo nna habari njema juu ya kiporo unachokula.


Je kuna umuhimu wa kutilia maanani rangi na ukubwa wa sahani katika kula ? Labda tujiulize, ni kwanini sahani zina rangi tofauti na mapambo ? Je ni swala la kuvutia tu macho au kuna kingine zaidi ?


Mwanaume 1 kati ya 3 wana matatizo ya nguvu za kiume – hii ni kulingana na utafiti uliofanyika. Upungufu wa nguvu za kiume unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na kufanya mazoezi.


"Watu pekee wenye mapenzi ya dhati ni wale wapendao chakula" - Nukuu toka uswazi 


Ilikuwa ni wikiendi moja nimetulia maskani ghafla nikapigiwa hodi na wageni watatu nyumbani. Ilikuwa mida ya kujaza tumbo na mie mkwanja nilionao haukuwa unapendeza kwa hiyo nisingeweza kuwapeleka sehemu kula, tatizo walikuwa mabinti.  Baada ya kutafakari kwa muda nikakimbilia dukani, nikachagua chakula rahisi kupika lakini kitakachopendeza. Nikanunua tambi (spaghetti) na kujifungia jikoni. Nikamwaga viungo tele. Nikachemsha tambi na kutengeneza mchuzi. Harufu ya viungo haidanganyi, ikawafikia wageni na mate yakawajaa mdomoni. Wanasubiria maanjumati ya haja, maana harufu siyo siri ilikuwa njema.


Mie  napenda misosi - kupika na kuila. Najua chakula ni kama hobby vile, bali ni bora zaidi. Mie napenda kujifunza na kujaribu mapishi tofauti. Na nikishajua mapishi huwa napenda kushirikisha marafiki na jamaa kuonja, na hapa nimepata pa kukutamanisha mapishi  yangu  - utanisoma tu. Mie siyo mtaalamu, bali nna ari ya kujifunza. Sina uzoefu wa muda mrefu kwenye mapishi bali nna dhamira ya kujifanza mapishi na kujaribu kuelezea kwa wale ambao hawajawahi kufikiria kuingia jikoni na kuanza kukaangiza. Nikiwa kwenye mapishi nakuwa serious kama nilivyo kwenye mapenzi, sitaki utani.

Nimepata bahati ya kukulia uswazi, na bado naishi uswazi - huku ndio maskani. Kwa mtazamo wangu, kukulia uswahilini ni bahati kubwa sababu unajifunza maisha tofauti angali mtoto. Ninachokipenda zaidi uswazi kwetu ni kuwa tunathamini kila kitu - hasa vile vinavyotakiwa kupewa thamani yake inayostahili, mfano chakula.  Huku kwetu watu tangu asubuhi hadi usiku wanawaza maakuli tu - Maisha ni kujiramba. Vilevile hakuna sehemu ambayo watu wanajua kula misosi mizuri kama uswazi. Kama huamini jiulize chips vumbi zinapatikana wapi? Je pweza wanauzwa wapi? Samaki wa kukaanga wanauzwa wapi? Mama ntilie wanapatikana wapi? Kuku wa kuchoma wanapatikana wapi?   Uswazi kwetu unapata kila kitu unachotaka bila tatizo. Kikubwa zaidi, vyakula vyote vya uswazi vinanukia na vitamu kupita maelezo, nadhani wewe jibu unalo.

Je unapenda misosi? Basi jumuika nami katika kuendeleza libeneke hili la misosi, uwe dada au kaka, mama au baba, mjomba au shangazi, wote tunajumuika hapa kwenye libeneke la misosi. Hakika tutafika, maana tukiwa wengi hakuna kinachoharibika - tutawekana sawa kwenye mambo yote ya kijamii, hasa maakuli na ustaarabu wa nyumbani. 

Karibu tujirambe pamoja yakhee, raha ya misosi sharti ni kushare na wenzio.